30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

COCA COLA KWANZA KUPUNGUZA UHABA WA MADAWATI

Na PENDO FUNDISHA-MBEYA


KAMPUNI ya vinywaji baridi kupitia kinywaji chake cha Coca Cola kwanza, imesema itaendelea kuisaidia Serikali kupunguza tatizo la uhaba wa madawati linalozikumba  baadhi ya shule za msingi na za sekondari.

Kampuni hiyo, imesema katika mwaka huu wa fedha, imetenga dawati 1,000 kwa shule za msingi na za sekondari mkoani Mbeya.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Basil Gadzios alisema imekuwa  ikitoa huduma kwa wanafunzi, watoto, wazee, mashirika na makampuni, hivyo ni vema nao wakarudisha fadhira kwa jamii  kupitia misaada mbalimbali.

“Kwetu hawa wote, ni wadau muhimu na nguzo pekee inachokiwezesha kiwanda hiki kuendelea,ni wajibu wetu  kurudisha asante  kwa jamii kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali hususani madawati,”alisema.

Alisema wanatambua changamoto zilizopo ndani ya jamii na kwamba Serikali peke yake haiwezi kuzitatua.

 Alisema mwaka jana, kampuni hiyo ilichangia dawati 500.

Mbali na madawati, pia Kampuni hiyo imesema itaendelea kujenga vituo vya polisi na kuboresha miundobinu ya barabara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles