24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

CLINTON AACHANA NA NDOTO ZA URAIS MAREKANI

WASHINGTON DC, Marekani


WAZIRI wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton amesema hatagombea urais wa taifa hilo.

Akizungumza katika mahojiano ya ana kwa ana na Kituo cha BBC redio 4 cha nchini Uingereza, Clinton alipoulizwa iwapo ana mpango wa kujitosa kwenye kuwania urais alisema hatagombea tena.

Clinton ambaye aligombea mara ya kwanza mwaka 2008 na kushindwa na Barack Obama katika mchujo ndani ya Chama cha Demoratic na Mwaka 2016 alishinda uteuzi wa ndani ya chama lakini aliangushwa na Trump katika uchaguzi uliofanyika Novemba 2016.

Katika uchaguzi wa 2016, Rais Trump alishinda kwa kupata kura 306 za majimbo ya uchaguzi  dhidi ya 232 alizopata Clinton ingawa mwanamama huyo alipata ushindi wa jumla kwa kumzidi Rais Trump kura milioni 2.9.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles