CIARA AKIRI KUMKOPI TIWA SAVAGE

0
442

NEW YORK, MAREKANI


NYOTA wa muziki wa Pop nchini Marekani, Ciara Harris, amethibitisha kukopi baadhi ya vitu kutoka kwenye wimbo wa Mnigeria,  Tiwa Savage.

Wiki iliyopita Ciara aliachia wimbo wake mpya ujulikanao kwa jina la ‘Freak Me’ ambao amemshirikisha Tekno, lakini unadaiwa wimbo huo umefanana na wa Tiwa Savage ambao aliuachia mwaka 2015 ukijulikana kwa jina la Before Nko.

Kutokana na hali hiyo mashabiki wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kumshambulia Ciara kwa kufanya hivyo, lakini mrembo huyo ameamua kuwajibu na kuweka wazi.

“Miaka mitatu iliyopita niliwahi kuusikia wimbo wa Tiwa Savage (Before Nko), ukweli ni kwamba ulinivutia, msanii huyo anaonekana kuwa na kipaji na nilipenda jinsi alivyoimba, hivyo ni kweli kuna baadhi ya vitu nimevikopi kutoka kwenye wimbo huo,” aliandika Ciara.

Hata hivyo Tiwa Savage hajaongea lolote juu ya mjadala huo ambao unaendelea kwenye mitandao ya kijamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here