24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Chuki za kisiasa zarejea Z’bar

vuaiNa Mwandishi Wetu, Zanzibar

HALI ya kisiasa visiwani Zanzibar imezidi kuwa tete baada ya kurejea kwa kasi chuki za kisiasa, huku wanawake wakijikuta wakipewa talaka na waume zao pamoja na kushamiri kwa vitendo vya hujuma katika miradi ya maendeleo.

Suala hilo linaibuka wakati Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ikiwa imetangaza uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika Machi 20, huku vyama tisa vikitangaza kutoshiriki kikiwamo Chama cha Wananchi (CUF).

Chuki hizo za kisiasa ambazo ziliibuka kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, zinarejea kwa kasi ambapo kwa sasa baadhi ya familia zimeanza kutengana ikiwamo hata kutonunua bidhaa katika maduka ya watu ambao wanaamini hawana uhusiano nao wa kisiasa.

Kutokana na hali hiyo, juzi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema hatua hiyo inaweza kuvirudisha visiwa hivyo katika chuki ambazo zilisahaulika baada ya kupatikana kwa mwafaka na hatimaye kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyovishirikisha vyama vya CCM na CUF.

Vuai alisema kwamba hivi sasa CCM inajiandaa kushiriki uchaguzi wa marudio licha ya baadhi ya vyama kuususia.

“Tunasikia baadhi ya vyama vikitangaza kutoshiriki ila ni lazima wananchi wajue kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa si ya CCM wala CUF, hivyo chama chochote kitakachoshiriki uchaguzi na kufikia matakwa ya kikatiba kitaunda Serikali ya umoja,” alisema Vuai.

Alisema ni lazima ZEC itangaze orodha ya vyama vitakavyoshiriki uchaguzi huo wa marudio kuliko kuendelea kukaa kimya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles