Imechapishwa: Wed, Sep 13th, 2017

CHUCHU HANS: NAANZA KUMWANDAA JADEN KUWA STAA 

Na KYALAA SEHEYE-DAR ES  SALAAM


STAA wa Filamu za Bongo, Chuchu Hans, amesema kuwa atafanya kazi kwa bidii kuhakikisha anamwandaa mtoto wake wa kiume kuwa staa wa baadaye.

Msanii huyo pamoja na Vicent Kigosi ‘Ray’ walifanikiwa kupata  mtoto wa kiume mapema mwaka huu, ambaye amepewa jina la Jaden.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Chuchu  alisema Jaden si wa kwanza, hivyo ili aweze kutimiza malengo yake ataingia mikataba na kampuni mbalimbali zitakazohitaji ubalozi wa mtoto huyo.

“Ifahamike mwanangu ni mtoto wa mastaa wawili hapa Bongo, hivyo namuomba Mungu aniweke ili niweze kumlea kifalme awe staa mkubwa na mwenye kuheshimika ndani na nje ya nchi,” alisema Chuchu.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

CHUCHU HANS: NAANZA KUMWANDAA JADEN KUWA STAA