30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

CHIZA ASHINDA KURA ZA MAONI CCM  

Na MWANDISHI WETU,KIGOMA


*Chadema, ACT waungana Buyungu

WAZIRI wa zamani wa Kilimo katika Serikali ya awamu ya nne, Christopher Chiza, ameshinda kura za maoni ndani ya CCM ikiwa ni maandalizi ya kuwania ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu, mkoani Kigoma utakaofanyika Agosti 12, mwaka huu.

Chiza ambaye aliwahi kuwa mbunge wa jimbo hilo aliibuka na ushindi katika mchakato wa kura hiyo iliyofanyika jana,  baada ya kupata kura 145 na kufuatiwa na Alyce Kamamba aliyepata kura 46, huku Emmanuel Gwegenyeza akipata kura 41.

Akizungumza baada ya kura hiyo Katibu wa CCM Wilaya ya Kakonko, Abdul Kumbuga, alisema wanachosubiri kwa sasa ni siku ya uchaguzi na kwamba wapiga kura ndio watakaoamua.

Hata hivyo taarifa za ndani zinaeleza kuwa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi inatarajiwa kukutana kesho jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine itapitia jina la mgombea huyo na kumtangaza baada ya taratibu za chama hicho kukamilika.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Chiza alishindwa kuteta nafasi hiyo baada ya kushindwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Mwalimu Kasuku Bilago kupitia Chadema, aliyefariki dunia Mei 26, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Wakati Chiza akishinda kura za maoni za kuwania ubunge Jimbo la Buyungu, vyama vya Chadema na ACT-Wazalendo vimekubaliana kusimamisha mgombea mmoja, Elias Kanjero (Chadema).

Kanjero aliibuka kidedea baada ya kupata kura 121 na kuwashinda wapinzani wake ambao ni Ashura Mashaka aliyepata kura 11 na Gaston Garibindi aliyeambulia kura 7.

Mgombea huyo anatarajiwa kutangazwa rasmi leo baada ya kupitishwa na Kamati Kuu ya chama hicho, iliyokutana juzi na jana jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), uchaguzi mdogo wa jimbo hilo utafanyika Agosti 12, 2018, sambamba uchaguzi wa kata 79 za Tanzania Bara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles