27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Chirwa: Azam itaandika rekodi mpya Kagame

Na Theresia Gasper -Dar -es-salaam

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Obrey Chirwa, amesema timu hiyo itahakikisha inatetea ubingwa wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu Kombe la Kagame.

Michuano ya Kombe la Kagame, itafanyika kuanzia Julai 7 hadi 21 mwaka huu nchini Rwanda.

Azam ndio bingwa mtetezi wa michuano hiyo, baada ya  kutwaa taji hilo mwaka jana, ilipoifunga Simba mabao 2-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ikiwa ni mara ya pili mfululizo, baada ya kufanikiwa kutwaa pia mwaka 2015.

Chirwa ameongeza mkataba wa mwaka mmoja wa   kuendelea kuitumikia Azam, baada ya ule wa awali kumaliza msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Baraa ulipofika tamati.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Chirwa alisema amejiandaa  kupambana ili kuhakikisha anaisaidia timu yake hiyo kutwaa ubingwa huo.

“Nimeshaongeza mkataba baada ya kufanya mazungumzo na kuelewana na viongozi wangu, kwa sasa tunajiandaa na michuano ya Kagame, binafsi nimejipanga kutoa mchango utakaowezesha kutwaa kutetea ubingwa,” alisema.

Akizungumzia ujio wa kocha Etienne Ndayiragije klabu kwake alisema yupo tayari kufanya kazi na kocha yeyote.

“Mimi kama mchezaji kazi yangu ni kucheza na si kuchagua kocha, nipo tayari kufanya kazi naye kuhakikisha  tunatwaa mataji,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles