28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

China yapiga marufuku pembe za ndovu

Grace Shitundu na Hadia Khamis, Dar es Salaam
SERIKALI ya China imetangaza kuzuia uingizwaji wa pembe za ndovu nchini humo kwa mwaka mmoja ili kudhibiti kushamiri kwa biashara hiyo.
Hatua hiyo imechukuliwa na China wakati taifa hilo na nchi nyingine za Bara la Asia zikilalamikiwa na dunia kwa kuwa na soko kubwa la meno ya tembo hivyo kuchochea ujangili duniani.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanyamapori duniani, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu aliipongeza China kwa uamuzi huo.
“China pamoja na nchi nyingine za Bara la Asia zilikuwa ni sehemu ya soko kubwa la biashara haramu ya meno ya tembo kwa hatua waliyoitangaza tunawapongeza na pia tunaomba nchi nyingine ziige mfano huo wa China,”alisema Nyalandu.
Hata hivyo waziri huyo alisema licha ya maadhimisho hayo, bado hali ya ujangili ni mbaya katika Tanzania.
Alisema Serikali inaandaa kikosi maalum cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na jeshi la Marekani kupata mafunzo ya namna ya kukabiliana na ujangili kwa njia za kisasa.
Hata hivyo alisema Tanzania inaongoza kwa kupokea watalii wengi katika nchi za Afrika Mashariki huku sekta ya utalii ikiliingizia taifa mapato ya Sh bilioni 2 kwa mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles