24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

China yalipiza kisasi kwa kuiongezea ushuru Marekani

BEIJING, CHINA

SERIKALI ya China imesema itaziwekea ongezeko la asilimia 25 la ushuru bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani zenye thamani ya dola bilioni 60 kuanzia Juni mosi.

Baraza la Ushuru na Forodha la nchi hiyo limesema hatua hiyo ni jibu kwa tangazo la Marekani la kuziongezea asilimia kama hiyo bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 200.

Utawala wa Rais Donald Trump umewaagiza maofisa wa biashara kutambua aina nyingine za bidhaa kutoka China zenye thamani ya dola bilioni 300 ili ziwekewe pia vikwazo vya ushuru.

Mazungumzo ambayo yamekuwa yakifanyika baina ya nchi hizo mbili zinazoongoza kiuchumi duniani kutafuta makubaliano ya kibiashara, yalivunjika Ijumaa iliyopita bila kufikiwa mwafaka.

Saa moja kabla ya China kutangaza ongezeko hilo la ushuru, Rais Trump alikuwa ameionya kutothubutu kulipa kisasi, la sivyo hali itakuwa mbaya zaidi. Lakini Wizara ya Mambo ya Nje ya China ilijibu kuwa nchi hiyo kamwe haitasalimu amri kwa shinikizo litokalo nje.                                                                                                                                   

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles