22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

CHEKA KUACHANA NA NGUMI

Na GLORY MLAY

BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Frances Cheka, amesema amebakiza miaka miwili kuachana na mchezo huo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Cheka alisema kutokana na machezo wa ngumi kutokuwa na masilahi, amebakiza miaka miwili kustaafu ili aweze kutafuta kazi ambayo itampa kipato kikubwa cha kuweza kujikimu pamoja na familia yake.

“Kwenye ngumi najipa miaka miwili tu, nikishindwa nageukia upande mwingine, kwanza mchezo huu hauna masilahi makubwa unaweza ukaenda nje ukapewa fedha  kidogo ambazo hazikidhi mahitaji, baada ya miaka hiyo miwili nitaangalia upepo unaenda wapi na nitaacha kabisa kazi hii ya ngumi,” alisema.

Alisema miaka hiyo miwili aliyojipa atahakikisha anarudisha kiwango chake alichokuwa nacho mwanzo baada ya kuanza kupoteza mwelekeo hivi karibuni.

Hivi karibuni Cheka alijikuta akipokea kichapo (TKO) katika raundi ya tatu  kutoka kwa bondia wa Poland, Dariusz Sek.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles