25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Chanzo cha watoto kuzaliwa na kichwa kidogo

mtoto-mwenye-kichwa-kidogo-akiwa-na-mama-yakeNa MWANDISHI WETU

MAKALA haya yanaeleza tafiti za wataalamu wa afya kuhusu athari za lishe duni, pombe kwa wajawazito pamoja na unene miongoni mwao.

Kwa kuanzia na lishe, watafiti wanasema kuwa awamu mbalimbali za maisha zinahitaji ulaji wa aina tofauti ya vyakula.

Kwa mtoto, mwili wake unahitaji virutubisho ili kusaidia ukuaji wa mwili, kama ni kijana mwili wake una mahitaji maalumu kwa ajili ya kuchochea makuzi.

Hali kadhalika wakati wa utu uzima huhitajika uzito uliolingana na mwili wa wastani.

Kwa upande wa wajawazito na wale wanaonyonyesha nao pia wana vyakula vyao maalumu wanavyohitaji tofauti kabisa na wanawake wengine.

Kwa mujibu wa tafiti za kitabibu, hali ya kiafya ya mjamzito huwa na athari mbalimbali kwa mtoto atakayezaliwa.

Hali kadhalika kuna ushahidi mkubwa kuwa magonjwa sugu ya watu wazima huanzia wakati mtoto akiwa bado tumboni mwa mama yake akiwa katika hali ya kiluilui (foetus).

Hivyo basi, wajawazito wanashauriwa kuzingatia vyakula wanavyokula kabla na baada ya kushika mimba.

Hebu tuangalie athari za chakula kwa afya ya mtoto na virutubisho vinavyopaswa kujumuishwa katika mlo wa mjamzito.

Chakula cha mjamzito kinaweza kuwa na athari kubwa muhimu kwa afya ya watoto kwa miaka mingi baada ya kuzaliwa.

Miaka ya hivi karibuni, Jarida la Masuala ya Lishe la Uingereza la Prestigious lilichapisha makala tatu kuhusu athari za lishe ya mjamzito kwa afya na ukuaji wa kiakili wa mtoto ambaye bado hajazaliwa.

Wengi wanafahamu fika  wajawazito wanapaswa kula chakula chenye virutubisho vyote vinavyohitajika ili kuhakikisha watoto wao watakaowazaa wamerutibika vya kutosha wakati wakiwa kwenye fuko la uzazi.

Hata hivyo, kile ambacho hakifahamiki kwa wengi ni kwamba chakula cha mjamzito kinaweza kuwa na athari chanya kwa afya ya watoto kwa muda wa miaka mingi, baada ya kuzaliwa.

Hivi sasa imethibitika kuwa kile kinacholiwa na akina mama wakati wa ujauzito, chakula ambacho kitakuwa kimejumuisha virutubisho vyote vinavyotakiwa, kinaweza kuwafanya watoto wao watakaozaliwa kuwa werevu zaidi.

Wataalamu wa afya wanasema kuwa hivi sasa wanaweza kuandaa kizazi kipya cha watoto werevu kwa kula chakula kinachotakiwa wakati wa ujauzito.

Wajawazito ambao katika kipindi cha ujauzito hawakupata lishe bora isiyo na protini, nishati, madini na vitamini kwa ujumla huzaa watoto walio na uzito wa chini.

Aidha, watoto hao huwa na uwezekano mkubwa wa kukumbwa na magonjwa ya kisukari katika kipindi cha utu uzima.

Ukiachana na umuhimu wa lishe bora kwa mjamzito na athari zake chanya kwa mtoto atakayezaliwa, tugeukie hatari ya unywaji pombe kwa akina mama hao.

Watu wengi wanafahamu madhara yanayotokana na utumiaji wa dawa za kulevya na ya kawaida pamoja na uvutaji sigara wakati wa ujauzito.

Hata hivyo, wanawake wengi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu madhara yanayosababishwa na unywaji pombe wakati wa ujauzito.

Utasikia mume au ndugu, jamaa na marafiki wakimshawishi mjamzito anywe japo kidogo ili kusherehekea mimba au kuburudika na mvinyo kidogo kwa madai chupa moja itamsisimua na haitamuathiri.

Maneno kama hayo ni ushauri usiofaa, ambao hauna faida yoyote bali athari mbaya kwa mtoto atakayezaliwa.

Unywaji pombe wa aina zozote wakati mama akiwa na mimba huwa na madhara tofauti kwa mtoto aliye tumboni mwake, kuanzia zile za wastani hadi kubwa.

Kumbuka kuwa mama anapokunywa pombe mtoto naye huinywa pia.

Kuna madhara makuu matatu yanayoweza kumsibu mtoto ambaye hajazaliwa bado iwapo mama yake alikuwa akinywa pombe wakati wa ujauzito.

Kwanza; ni kuwapoo hatari kubwa ya kutoka mimba au kuzaliwa mtoto kabla ya miezi tisa. Pili; chembe za mwili za mtoto aliye tumboni zinaweza kuathiriwa au anaweza kuwa na uzito mdogo na kuzaliwa akiwa na ulemavu zaidi ya mmoja.

Tatu; chembe za ubongo wa mtoto huyo zinaweza kuharibiwa na pombe na mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ambayo kitaalamu huitwa Foetal alcohol syndrome.

Miongoni mwa madhara yanayoweza kumpata mtoto ni kama vile kuzaliwa akiwa na ulemavu wa kimwili na kiakili.

Kwa upande wa kimwili, mtoto huweza kuathiriwa na mtindio wa ubongo, anaweza kuzaliwa akiwa na kichwa kidogo na uso wake kuwa na mwanya mkubwa baina ya pua na mdomo.

Kwa upande wa macho, wengine huzaliwa wakiwa na matatizo ya kuona, masikio hushambuliwa na baadhi ya magonjwa.

Kwa hivyo ni jambo lenye umuhimu kwa akina mama kuwaandalia watoto wao mwanzo mzuri wa makuzi bora tangu wakiwa tumboni.

Kw upande wa unene, una uwezekano wa kusababisha hatari kubwa ya saratani ya matiti kwa wanawake.

Wanawake wanaoongezeka uzito kupita kiasi katika utu uzima, wanakabiliwa na hatari kubwa na ya muda mrefu ya kukumbwa na saratani za matiti.

Uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa, uzito na saratani ya matiti vinaweza kuwa na uhusiano wa karibu.

Utafiti uliofanywa kwa akinamama zaidi ya 44,000 nchini Marekani umeonyesha kuwa, kadiri mwanamke anavyozidi kunenepa, ndivyo anavyozidi kujiweka katika hatari ya kukumbwa na saratani za aina mbalimbali, tena katika hatua zake zote.

Hatari ya saratani ya matiti imehusishwa na ongezeko la viwango vya homoni ya estrojeni na tishu za mafuta zinazozalisha homoni hiyo.

Hivyo basi, akina mama wanashauriwa kuboresha uzito wa mwili kwa kufuata misingi ya afya katika kipindi chote cha utu uzima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles