31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

CHANJO YA SARATANI YALETA MAFANIKIO KILIMANJARO

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Chanjo dhidi ya Saratani ya kizazi (HPV) iliyotolewa kwa  wasichana 135,700 mkoani Kilimanjaro imeonesha mafanikio kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 70.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema hayo leo Jumanne Aprili 27, jijini Dar es Salaam katika mkutano wake na viongozi wa dini na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu uhamasishaji na uraghibishaji wa chanjo hiyo.

“Chanjo hiyo wamepewa kuanzia mwaka 2004 hadi 2017,  na imeonyesha mafanikio ambapo sasa wamepata uelewa wa chanjo hiyo na wanaenda wenyewe pindi wakisikia inaanza kutolewa.

“Katika awamu ya kwanza walipewa watoto 76,000 na awamu ya pili walipewa watoto 59,700, kwa mafanikio hayo tunakusudia kuwafikia watoto 616,734 ndani ya mwaka 2018 pindi tutakapoizindua Aprili, mwaka huu,” amesema.

Amesema chanjo hiyo imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na TFDA kwamba ni salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles