23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Chanjo ya Ebola kutolewa Uganda

kampala, uganda

SERIKALI ya Uganda kupitia Wizara ya Afya, imetangaza kufanya kampeni ya kuwapatia chanjo wananchi wake kama sehemu ya kuwakinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola.

Hatua hiyo imeungwa mkono na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), kutokana na sababu ya tishio la kusambaa kwa ugonjwa huo kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Tishio la kusambaa kwa ugonjwa huo hadi nchi zinazopakana na nchi hiyo ya DRC linazidi kuongezeka, hasa upande wa Mashariki ulipo mji wa Beni.

Hii ni kutokana na ukosefu wa usalama na hivyo kukwamisha jitihada za kupambana na ugonjwa huo kama ilivyotokea siku za karibuni ulipozuka na kusababisha vifo vya watu 179.

Na kwa naana hiyo, mikoa iliyo jirani na mpaka wa nchi za Burundi, Rwanda na Uganda iko hatarini.

Kutokana na hali hiyo, Uganda ndipo ilipoamua kuchukua hatua za makusudi na za awali kukabiliana na ugonjwa huo wa Ebola.

Chanjo hiyo itagawiwa kama kinga ya kuzuia kwa mtu binafsi, wakiwamo wafanyakazi wa afya walioko mstari wa mbele vitani, timu za ufuatiliaji na za mazishi.

Mwakilishi kutoka Serikali ya Uganda kwa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, Dk. Yonas Woldemariam, ameviambia vyombo vya habari kuwa kiwango cha zaidi ya chanjo 2000 vimekwisha kupatikana.

Timu zinazoshughulika na chanjo zimepelekwa upande wa magharibi wa nchi ya Uganda karibu na mpaka baina yake na nchi ya D.R. Congo, ili kuanza kazi katika wilaya tano zilizoko hatarini zaidi.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia, chanjo hiyo ilikuwa ikitolewa maalumu kwa watu wote waliowahi kuwa karibu na wagonjwa waliothibitika kuathiriwa na ugonjwa wa Ebola.

Uganda imeendelea kuchukua hatua nyingine kama vile uchunguzi wa watu wanaovuka kutoka katika maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu karibu na mpaka baina yake na nchi ya DRC tangu mwezi wa Agosti mwaka huu.

Nchi hiyo ya DRC, ina sifa ya kujibu haraka dharura za kiafya. Mnamo mwaka 2000, ilipata maambukizi ya Ebola yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya mia mbili. Na tangu wakati huo, iliimarisha ufuatiliaji wake na timu za kukabiliana na dharura kwa kutambua mapema viashiria vya kuzuka kwa virusi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles