23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

CHADEMA YAITA KIKAO WABUNGE, MADIWANI

Na ELIZABETH HOMBO-DAR ES SALAAM


SIKU moja baada ya viongozi wakuu wa Chadema kufikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka manane, Kamati Kuu ya chama hicho imesema bado wana imani na baadhi ya mahakimu wenye moyo wa kutenda haki.

Juzi, viongozi hao wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe walisomewa mashtaka, wakakosa dhamana na kupelekwa Gereza la Segerea hadi leo mahakama itakapotoa uamuzi wa kupewa dhamana au laa.

Akisoma maazimio ya Kamati Kuu iliyokutana jana Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari, alisema wamekutana kwa dharura na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo kujadiliana kuhusu viongozi wao kuwekwa mahabusu.

Alisema leo baada ya uamuzi wa mahakama, Kamati Kuu itakutana tena na kwamba baadaye itakutana na wabunge na madiwani wote wa chama hicho kutafakari mustakabali wa demokrasia nchini na mambo yanayoendelea.

“Leo tumekutana kwa dharura na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, kesho (leo) baada ya maamuzi ya mahakama kuhusu viongozi wetu, tutakutana tena kutafakari na baadaye Kamati Kuu, wabunge na madiwani watakutana kujadili mustakabali wa demokrasia nchini na kutoa maelekezo kwa wanachama wake nini cha kufanya.

“Kwahiyo tunatoa wito kwa wadau wote wa demokrasia nchini, kama vile viongozi wa dini walivyofanya na tunategemea Bakwata (Baraza Kuu la Waislamu Tanzania) nao watafanya hivyo kushiriki kikamilifu katika mapambano ya kudai demokrasia kwa ustawi wa wananchi wote nchini,” alisema Profesa Safari.

 

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles