28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Chadema watinga ofisi ya mkurugenzi na fomu za pingamizi

Derick Milton, Simiyu

Zaidi ya wagombea 100 ngazi ya vijiji na vitongoji kupitia chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema) wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, wamelazimika kufika katika ofisi ya Mkurugenzi wa halmashuari hiyo kwa ajili ya kuonana na Msimamizi wa uchaguzi Wilaya.

Wagombea hao ambao hawakuteuliwa kugombea nafasi hizo, walifika katika ofisi hiyo ili kuwasilisha malalamiko yao juu ya hujuma walizofanyiwa na wasimamizi wasaidizi, ikiwemo kutopokelewa kwa fomu zao za pingamizi la kutoteuliwa.

Akiongea mbele ya Msimamizi wa Wilaya Amina Mbwambo kwa niaba ya wagombea hao, Katibu wa chama hicho Wilaya, Goleha Lazaro amesema wamefikia uamuzi huo kutokana na wasimamizi wasaidizi wa maeneo yao kukataa kupokea fomu hizo kinyume na utaratibu.

Amesema wasimamizi hao walidai kuwa wao hawawezi kupokea fomu za pingamizi mpaka wapate maelekezo kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi wilaya hali ambayo ni kinyume na kifungu namba 23 cha sheria ya uchaguzi.

“Sasa tumekuja kwako msimamizi wa uchaguzi wilaya tunataka ufafanuzi ni wapi kwenye sheria inasema wasimamizi wasaidizi wanatakiwa kupata maelekezo kutoka kwako ili wapokee fomu za pingamizi?,”  amehoji katibu huyo.

Msimamizi huyo amewaeleza kuwa wasimamizi wasaidizi hawatakiwa kukataa kupokea fomu hizo, na wala hakuna kipengele kwenye sheria ya uchaguzi huo kinachosema lazima wapate kwanza maelekezo kutoka kwake.

Ameongeza kuwa kama yupo msimamizi msaidizi anayekataa kupokea fomu hizo, anakiuka sheria za kanuni za uchaguzi huo.

Amewataka kurudi kwa wasimamizi hao na kupeleka fomu hizo, huku akiwahakikishia malalamiko hayo kuyafanyia kazi mara moja na fomu zao zipokelewe kabla ya muda haujaisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles