27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Chadema wasusia uchaguzi Serikali za Mitaa kisa rafu kwa wagombea wake

Ramadhan Hassan, Dodoma

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimejitoa kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku kikiwataka wagombea wake waliochezewa rafu kuacha kukata rufaa.

Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amatangaza uamuzi huo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa ambapo amesema sababu kubwa ni wagombea wa chama hicho kuenguliwa kwa sababu mbalimbali.

Mbowe amesema mara baada ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho na wabunge, maazimio waliyokubaliana ni kugomea uchaguzi huo sababu majina ya wagombea wengi kukatatwa.

“Sisi kama chama tumeamua hatutashiriki zoezi hili na ninatoa amri kama Mwenyekiti wa viongozi na wagombea nchi nzima wasitishe kugombea na wasitishe kukata rufaa.

“Waachane na kuweka mapingamizi hatupo tayari kubariki ubatili, huu ni uhuni, wananchi wana hasira na wana haki ya kuwa na hasira na waendelee kuwa na hasira,” amesema Mbowe.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles