24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Chadema waitaka serikali kutotumia jina, nembo ya chama chao

Faraja Masinde, Dar es Salaam

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetaka Serikali kutotumia nembo na jina la chama hicho kwenye karatasi za kupigia kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, mwaka huu.

Naibu Katibu Mkuu (Bara), wa chama hicho, John Mnyika amesema amesema hayo leo Jumapili Novemba 10, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema sababu ya uamuzi huo ni kutokana na wao kujiengua katika kinyang’anyiro hicho hivyo wagombea wao wasiwepo katika fomu hizo za kupigia kura.

“Kesho Novemba 11, tutamuandikia barua Waziri wa Tamisemi (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Suleiman Jaffo, kuacha kutumia jina nembo ya chama chetu.

“Pia tunamuomba Rais Dk. John Magufuli, kuingilia kati ukiukwaji wa sheria unaoendelea kwenye uchaguzi huo kama alivyohamasisha wakati wa uandikishaji,” amesema Mnyika.

Kauli ya Mnyika imekuja siku chache baada ya chama hicho kujitoa kushirikia katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa madai ya ukiukwaji wa sheria ikiwamo baadhi ya wagombea kuenguliwa kutokana na kasoro mbalimbali katika ujazaji fomu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles