25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Chadema Mtwara wamvaa Jaji Mutungi

Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Na Florence Sanawa, Mtwara

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mtwara,  kimemtahadharisha Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kuacha kuingilia katiba ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa chama hicho mkoani hapa, Kassim Bingwe, alisema msajili wa vyama alitoa taarifa zenye lengo hasi kwa ukuaji wa demokrasia nchini.

Alisema Jaji Mutungi kuingilia shughuli halali za chama hicho ni kinyume cha majukumu ya ofisi yake kwa mujibu wa sheria na matarajio ya wananchi katika kujenga demokrasia nchini.

“Msajili anatambua kuwa huu ni ubakaji wa demokrasia na pia anaendelea kutolea hoja mambo yasiyo na mashiko huku akinyamazia mambo yanayolalamikiwa kukwaza demokrasia nchini.

“Licha ya msajili kudai amepokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA wakiwemo waliofukuzwa, iweje ayatoe leo kwenye vyombo vya habari huku akijua kuwa kifungu kinacholalamikiwa kilifutwa na katiba mpya ya 2006?” alihoji.

Bingwe aliongeza: “Hivi msajili ameshindwa kuona kuwa wanachama wa chama cha CCM wameanzisha na kuendeleza kampeni za uchaguzi wa 2015 kabla ya wakati huku akijua kuwa hilo ni kinyume cha Katiba na sheria ya uchaguzi?” alihoji.

Bingwe alisema inaonekana msajili huyo haoni vijembe vya makundi ndani ya CCM kugombea uongozi kwenye chama chao kabla hata ya muda jambo lililosababisha baadhi yao kuadhibiwa.

Anaongeza kuwa kitendo cha msajili kutamka kuwa mazuio kwa uongozi wa CHADEMA kujihusisha na mambo ya chama kumezua mtafaruku miongoni mwa wanachama na miongoni mwa wapenda chama, hivyo kuwaweka katika hali tete.

“Jambo hili limetusababishia usumbufu wa kujibu mambo yasiyo na tija kwa jamii huku tukiacha kutekeleza majukumu ya ndani ya chama na jamii katika ujenzi wa demokrasia na uchumi wa jamii,” alisema Bingwe.

Hivi karibuni msajili alinukuliwa akizungumza na vyombo vya habari akikaripia na kuwazuia viongozi wakuu wa Chadema kutogombea tena nyadhifa zao, kwani kwa kufanya hivyo ni kuvunja katiba ya chama hicho.

- Advertisement -

Related Articles

3 COMMENTS

  1. Ni vema viongozi wetu wakatofautisha utumishi na siasa!! hajaona kabisa yanayoendelea ccm? au ndicho kimemtuma avuruge demokrasia ya CHADEMA??

  2. Tunaomba mtafaruku huu ufanyiwe marekebisho kwan tunakoenda sio sahihi kwani chama chenye nguvu na viongoz wake wasiingilie kati demokrasia ya chama kisicho na nguvu kwan hii inasababisha uonevu na inasabiabisha watu washindwe kuwa na 7uhuru wa kidemokrasia

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles