27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Chadema kutoa tamko zito leo

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI  wa Chama  Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, leo  anatarajiwa kutoa maazimio mazito ya Kamati Kuu ya  chama hicho iliyokutana kwa siku mbili, Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa   Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema, ilisema pamoja na mambo mengine, kamati hiyo ilijadili kwa kina hoja tatu za msingi.

Alitaja hoja hizo kuwa ni hali ya mwenendo wa  siasa na ukandamizaji wa demokrasia, kuporomoka kwa uchumi na hali ngumu ya maisha inayowakabili Watanzania.

Alisema  hoja ya tatu ni kamatakamata inayoendelea kufanywa na vyombo vya dola  dhidi ya viongozi, wanachama na wafuasi  wa chama hicho katika maeneo mbalimbali.

“Pamoja na  mambo niliyotaja hapo juu, tunategemea mwenyekiti wetu atatoa maelezo mengi kesho (leo), atakapokutana na waandishi wa habari makao makuu.

“Tuna mambo mengi mno, kumekuwapo na tatizo la viongozi wetu wengi kukamatwa kila kukicha maeneo mbalimbali, sisi kama chama cha upinzani hatuwezi kunyamazia jambo hili,” alisema Mrema.

Moja ya matukio ambayo yalitikisha nchi hivi karibuni ni kukamatwa kwa Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi  kuwa “Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli ni ya ubaguzi wa ufamilia,ukabila, ukanda na udini.”

Kutokana na tuhuma hizo, alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka ya uchochezi.

Baada ya kupewa dhamana Lissu alisema hakuna gereza likalowanyamazishwa  mahabusu na  kwamba wataendelea kuzungumza siku hadi siku hadi kifo kitakapowachukua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles