26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

CEED yawafunda wajasiriamali usimamizi wa biashara

Ramadhan Hassan, Morogoro

Kituo cha Ujasiriamali cha CEED Tanzania, kimetoa mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa biashara kwa wajasiriamali mkoani Morogoro yaliyolenga  kuwawezesha namna ya kusimamia biashara zao.

Pamoja na mafunzo hayo pia kimetoa mafunzo ya namna ya kutatua changamoto za kibiashara na fursa mbalimbali mkoani humo.

Akizungumza na wajasiriamali wa mkoani Morogoro, jana Mkurugenzi wa CEED Tanzania,  Atiba Amalile aliwakumbusha wajasiriamali hao kufanya kazi kwa juhudi pamoja na kujifunza kwa wengine.

Naye Mshauri wa  masuala ya kodi na Mwakilishi wa CEED Tanzania mkoani Dodoma, Baptist Mnyalape amewahimiza wajasiriamali hao kuhakikisha wanafahamu kanuni zinazoweza kuathiri biashara zao moja kwa moja.

“Naomba niuwakumbushe tu ndugu zangu wajasiriamali kuhusu kuzingatia masuala mazima ya kodi, tuhakikishe tunafahamu kanuni na sheria ambazo zinaweza kuingilia na kuathiri biashara zetu moja kwa moja, ukishindwa kuzingatia haya itagharimu muda wako pamoja na pesa zako,” amesema Mnyalape.

Kwa upande wa mwakilishi kutoka Benki ya CRDB, Dennis Kayanda amewasisitiza wajasiriamali hao juu ya umuhimu wa kufuata sheria ya matumizi ya ushuru wa ardhi.

“Ni hatari zaidi kwa kutafuta mikopo kutoka benki za biashara na kuwekeza katika biashara ambazo zinaweza kuwa hazifanyi kazi katika eneo hilo na hivyo kuathiri biashara,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shambani Milk mkoani Morogoro amesema ameyafurahia mafunzo hayo na kwamba yatawasaidia jinsi ya kuendesha biashara zao.

“Nimekuwa nikihudhuria mara kwa mara mafunzo ya CEED, mfano mafunzo yaliyokuwa yakitolewa jijini Dar es Salaam yamenisaida kujua habari za biashara bora, namna ambavyo mtu unawezakutumia teknolojia kujifunza namna ya kuendesha biashara yako,’’amesema Mfinanga.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na wajasiriamali mbalimbali wa mkoani Morogoro pamoja na viongozi wa Benki za CRDB, NMB NBC, Azania na Benki ya Afrika ambazo kwa pamoja zimewapa elimu wajasiriamali jinsi ya kupata mikopo bila shida na namna ya kutumia mikopo hiyo kukuza biashara zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles