27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

CCM YAWAVUTIA KASI WALIOTWAJWA ESCROW

Na EVANS MAGEGE-DAR ES SALAAM

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema  a kinasubiri uchunguzi wa makada wake   wanaodaiwa kuhusika kwenye kashfa ya usafirishaji wa mchanga wa madini (makinia) na uchotaji wa fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.

Kauli hiyo ilitolewa jana kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba Dar es Salaam na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, alipozungumza na waandishi wa habari.

Polepole alisema kwa sasa chama hicho kinasubiri uchunguzi unaofanywa na vyombo vya dola.

Alisema ikithibitika   makada hao wamekutwa na makosa CCM itafanya haraka uamuzi ambao hakuutanabaisha kama utakuwa  wa kuwatimua uanachama au la.

“CCM tunasubiri kwa hamu kubwa uchunguzi dhidi yao na ikithibitika tutafanya haraka kuchukua uamuzi,” alisema Polepole.

Wakati Polepole akitoa kauli hiyo, gazeti moja la kila siku(si Mtanzania) katika toleo lake la jana, liliripoti kuwa makada hao wamezuiliwa kuwania nafasi zozote za uongozi ndani ya chama hicho.

Pia   taarifa kutoka kwenye mifumo ya ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa makada hao wapo hatarini kuvuliwa uanachama.

Kwamba chama hicho kimechoka  kubeba lawama kwa makada wake kuhusika na kila aina ya ufisadi unaoibuka.

Taarifa hizo  zinaeleza kuwa wabunge na mawaziri  waliotajwa kwenye kashifa hizo wataenguliwa uanachama  hivyo kupoteza ubunge kabla ya muda wao kumalizika.

Hata hivyo gazeti hili lilipomuuliza Polepole juu ya madai hayo hakukubali au kukataa  badala yake akamwahidi mwandishi wa habari hiyo kuwa suala hilo angelizungumzia kwenye mkutano na wanahabari  a jana.

Makada wa CCM wanaotuhumiwa kwa kashfa ya Escrow ni pamoja na wabunge  William Ngeleja (Sengerema), Andrew Chenge(Bariadi), Profesa Anna Tibaijuka(Muleba Kusini), Profesa Sospeter Muhongo(Musoma Vijijini) na Victor Mwambalaswa (Lupa).

Makada wanaotuhumiwa kwenye suala  la makinikia ni Chenge, Ngeleja, Profesa Muhongo, Mbunge wa Igunga, Dk.Dalaly Kafumu, Daniel Yona na Nazir Karamagi.

Polepole pia alisema kuwa CCM  kinaridhika na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Rais, Dk. John  Magufuli ya kuipeleka nchi katika uchumi wa kati kupitia sera ya viwanda.

Katika muktadha huo alisema chama hicho kinaunga mkono kauli ya Rais ya kutowaruhusu wanafunzi waliopewa ujauzito kuendelea na mfumo rasmi wa elimu.

Kwa ufafanuzi wa kina, Polepole alisema suala la elimu limegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni mfumo rasmi na mfumo usio rasmi.

Alisema mfumo rasmi ni ule wa mtoto kusoma darasa la kwanza mpaka la saba, kuendelea kidato cha kwanza mpaka cha nne, kitado cha tano hadi sita na kuendea na elimu ya juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles