31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

CCM YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA ILANI  

Na Ibrahim Yassin,Nkasi


ccmHALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, imeipongeza Serikali kwa utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

Pongezi hizo zilitolewa jana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Nkasi,Desderius Mipata baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya, Said  Mtanda ambaye alisema ilani hiyo inatekelezwa kwa vitendo.

Alisema baadhi ya mambo yaliyofanywa yanaonekana kwa macho ni pamoja na kuendelea na kazi ya kuwabana watumishi wasiokuwa  waaminifu.

Alisema suala la upatikanaji wa pembejeo,ukamilishaji wa miradi kadhaa ya maji ya mamilioni ambayo imegharimu mamilioni ya fedha ilisimama, lakini sasa inaendelea,ujenzi wa zahanati,vituo vya afya na upatikanaji  wa dawa.

Alisema wamekuwa wakihamasisha watu kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),utekelezaji wa utengenezaji wa madawati,ujenzi wa vyumba vya madarasa na miundombinu.

Alisema katika utekelezaji wa miradi mingi kama ambavyo wameelekezwa na ilani ya chama kuna baadhi imekwenda vizuri, lakini mingine ilikuwa na changamoto kadhaa.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Zeno  Mwanakulya aliwataka watendaji wa Serikali kukubali mabadiliko ya utendaji chini ya falsafa ya ‘’hapa kazi tu,’’ huku akimsihi mkurugenzi kuendelea kuwachukulia hatua watendaji ambao si waadilifu.

Mbunge wa  Nkasi Kasikazini, Ally Kessy (CCM), alisema watahakikisha  watumishi wasiowaadilifu wanachukuliwa hatua papo hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles