24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

CCM WAMSHUKIA MAKONDA

PATRICIA KIMELEMETA – Dar es Salaam


CHAMA CHA Mapinduzi (CCM) kimesema kimeshangazwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuwafanyia sherehe   polisi waliosimama uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ukonga Jumapili iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana, Katibu, Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, alisema Makonda hakupaswa kufanya hivyo.

Alisema hiyo ni  kwa sababu baadhi ya askari waliona vitendo vya ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi vinafanyika lakini walikaa kimya.

Juzi Makonda alikutana na polisi waliosimamia uchaguzi huo na kuwapongeza kabla ya kunywa nao soda huku wakishangilia kwa kuimba na kumbeba juu juu mkuu huyo wa mkoa.

Jana, Polepole alisema ilikuwa mapema mno kwa Makonda kuandaa sherehe kama hiyo kwa sababu uchaguzi ulighubikwa na dosari ndogondogo ambazo askari hao walishindwa kuzidhibiti.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles