25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

CCM: MCHUNGAJI MSIGWA JIANDAE KUNG’OKA

NA RAYMOND MINJA, IRINGA                  |                       


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Mjini, kimesema   Mbunge wa jimbo hilo, Mchungaji Peter Msigwa ajiandae kisaikolojia kuachia jimbo hilo.

Chama hicho kimesema hali hiyo  inatokana na wimbi là madiwani wa Chadema waliohama na baada ya uchaguzi mdogo wamepoteza kata zote.

Katika uchaguzi mdogo uliomalizika hivi karibuni, CCM kilifanikiwa kuchukua kata tano bila kupingwa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Iringa, Joseph Mgongolwa alisema ushindi walioupata ni salamu tosha kwa Mchungaji Msigwa kujitafakari na kuangalia kazi nyingine ya kufanya kwa sababu hatarudi  mwaka  2020.

Alisema sasa umefika muda wa kuwatumikia wananchi wa Iringa na si  muda wa kufanya siasa zisizotekelezeka na za kupiga kelele majukwaani.

Alisema wana Iringa wa sasa ni watu wanaohitaji mabadiliko na maendeleo, lakini kumekuwapo na watu wanaokwamisha juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Dk. John  Magufuli, hivyo ni vema wakaacha siasa.

“Ule muda wa kupiga kelele umekwisha, sasa ni vitendo, Watanzania wamechoka kudanganywa… wana Iringa wamechoka  ahadi hewa, wanataka mabadiliko,”alisema.

Alisema umefika wakati wa kufanya siasa za kutenda zaidi kuliko siasa za vijembe na matusi ili kumkomboa Mtanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles