25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

CCM Handeni watishia kutomnadi mgombea ubunge

NA MWANDISHI WETU, TANGA

WAGOMBEA 15 waliojitokeza kuomba ridhaa ya kuwania ubunge Jimbo la Handeni Vijijini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), wametishia kutomnadi mgombea aliyeshinda kura za maoni, John Saru, kwa madai kuwa ushindi wake ulitokana na uchakachuaji wa matokeo akisaidiwa na uongozi wa wilaya.

Walisema iwapo ataidhinishwa na vikao vya juu vya chama kupambana na wagombea wengine wa vyama vya upinzani, hawatampa ushirikiano badala yake watamuunga mkono mgombea wao wa nafasi ya urais pekee.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mmoja wa wagombea hao, Chifu Msopa, alisema ushindi aliopata Saru katika kura za maoni haukuwa halali ndiyo maana hadi sasa wamegoma kuweka saini ya kukubali matokeo.

Alisema wanaviomba vikao vya juu vya CCM kutoa tamko juu ya matatizo yaliyojitokeza wilayani Handeni kwani uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya rushwa ambavyo vilinyamaziwa na uongozi husika.

“Mgombea wetu wa urais, John Magufuli atapata kura za kishindo, lakini ubunge hatutampa Saru endapo chama kitampitisha kwani ushindi wake si halali na umejaa ukiukwaji mkubwa, hivyo tunakiomba chama kifanye uchunguzi na kiwapitishe wagombea wanaokubalika hapa jimboni,” alisema Msopa.

Katibu wa CCM wilayani humo, Saleh Kikwehu, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo, alisema wanaendelea na vikao kusikiliza malalamiko hayo huku akisema yeye si msemaji wa suala hilo kwakuwa hivi sasa lipo katika ngazi ya mkoa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles