CBT YAJITOA KUDHAMINI UZALISHAJI MICHE YA KOROSHO

0
448

|Hadija Omary, LindiMkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amezitaka halmashauri zote za mkoa huo, kufanya maandalizi ya kutosha kuzalisha miche mipya ya korosho katika msimu wa mwaka 2018/19 kutokana na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), kushindwa kuendelea kudhamini kuzalisha miche hiyo.

Zambi ameyasema hayo juzi katika kikao cha maandalizi ya ununuzi wa zao la korosho kwa msimu wa mwaka 2018/19, kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa zao hilo wakiwamo wakuu wa wilaya, wakurugenzi, viongozi wa vyama vya ushirika,  taasisi za kibenki, wakulima na wanunuzi wa zao hilo.

“Katika misimu miwili mfululizo Bodi ya Korosho ilikuwa inadhamini uzalishaji wa miche ya mikorosho kupitia katika Chuo cha Kilimo cha Naliendele, mkoani Mtwara kwa kutoa mbegu bora za zao hilo pamoja na vifaa vya kuzalishia, hivyo ni lazima halmashauri zikafanya maandalizi ya kuotesha mapema kwa kuwa waliokuwa wanasimamia uzalishaji huo hawatafanya tena,” amesema.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi  Mkuu wa CBT, Mhandisi Salum Buriani amesema licha ya bodi hiyo kutojihusisha na udhamini wa uzalishaji wa miche ya mikorosho kwa  msimu huu, pia bodi hiyo haitahusika katika ununuzi wa magunia ambapo jukumu hilo wamelikasimisha katika vyama vikuu vya ushirika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here