Imechapishwa: Tue, Apr 17th, 2018

CARDI B AONESHA UWEZO COACHELLA

CALIFONIA, MAREKANI


MWANAMUZIKI wa hip hop wa Marekani, Cardi B, juzi ameonesha kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki wake katika sherehe  za Coachella zilizofanyika Ukumbi wa Empire Polo uliopo jijini Califonia, Marekani.

Cardi B ambaye ni mjamzito, alipanda jukwaani kuonesha uwezo wake wa kutoa burudani ikiwa ni siku moja tangu mwanamuziki, Beyonce apande kuungana tena na kundi la Destiny’s Child.

Gumzo kwa mwanamuziki huyo liliongezeka baada ya kuvaa nguo iliyobuniwa na Alejandro sawa na kundi la  TLC. Nyota huyo pia alitumbuiza pamoja na kundi la YG, G-Eazy, Chnace The Rapper, Kehlani na 21 Savage.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

CARDI B AONESHA UWEZO COACHELLA