Cardi B amjaribu Minaj kwa Meek Mill

0
809

MIAMI, MAREKANI

Staa wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Belcalis Almánzar ‘Cardi B’, amepanga kuachia wimbo mpya aliomshirikisha mpenzi wa zamani wa Nicki Minaj, Meek Mill.

Cardi B na Nicki Minaj wamekuwa kwenye mgogoro kwa miezi kadhaa sasa, lakini Cardi B anaonekana kutaka kuendeleza bifu lao baada ya kutangaza kuwa anataka kuachia wimbo na aliyekuwa mpenzi wa msanii huyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Cardi B na Meek Mill wamekamilisha wimbo wao ambao unajulikana kwa jina la ‘Hooks and Verses’, hivyo mashabiki wa msanii huyo wanausubiri kwa hamu kubwa.

Hata hivyo, hajaweka wazi kuwa kazi hiyo ataiachia lini lakini mashabiki wanaamini wimbo huo utazidi kuchochea bifu la warembo hao ambao wanafanya muziki wa hip hop.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here