30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

California yakumbwa na tetemeko kubwa kuwahi kutokea ndani ya miaka 20

Andy Randolph na mtoto wake William wakiwa wamesimama kwa ajili ya kuchukua picha ya barabara iliyopasuka kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea California.

CALFONIA-MAREKANI

TETEMEKO kubwa la ardhi kuwahi kutokea ndani ya kipindi cha miaka 20, limepiga kusini mwa mji wa California.

Mbali na California  baadhi ya maeneo ya Nevada nchini Marekani nayo yalikumbwa na tetemeko kama hilo.

Tetemeko hilo lilitokea juzi wakati Marekani ikiadhimisha siku yake ya uhuru na kusababisha majeruhi na uharibifu na kutokana na  matetemeko mengine madogo ya ardhi.

Wakati baadhi ya vyombo vya habari vikiripoti kuwa tetemeko hilo lilikua na  na ukubwa wa 7.1  katika kipimo cha Richter vingine viliripoti  ukubwa wa 6.4 ambalo lilipiga jangwa la Mojave, umbali wa kilomita 240 kaskazini mashariki mwa Los Angeles, karibu na mji wa Ridgecrest, California.

Mtaalamu wa miamba, Dk. Lucy Jones alisema tetemeko hilo linaweza kuendelea.

“Hili ni tetemeko ambalo linaweza kuendelea,” alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari.

“Kila tetemeko linaweza kufanya tetemeko jingine,” alisema na kuongeza kuwa kulikuwa na uwezekano wa asilimia 10 wa tetemeko kama hilo au zaidi ya hilo  kutokea wiki ijayo.

Tetemeko hilo mbali na kuathiri Las Vegas na jimbo jirani la Nevada pia limeathiri maeneo ya mpakani na Mexico.

Gavana wa California, Gavin Newsom  alitoa msaada wake kwa watu alioathirika na tetemeko hilo, na kutoa wito kwa Rais kutangaza hali ya dharura pamoja na kutoa misaada.

Mkuu wa kikosi cha zimamoto, David Witt amethibitisha watu kadhaa kujeruhiwa na kwamba nyumba zilishika moto katika mji huo ulio na wakazi elfu 28.

Timu ya dharura ya uokoaji iliukabili moto mdogo, uvujaji wa gesi na ilikuwa ikishughulikia ripoti za barabara zilizopasuka kutokana na tetemeko hilo.

“Tumepata matatizo ya moto, gesi zimevuja, kuna majeruhi, watu hawana umeme, tunafanyia kazi yote kadiri inavyowezekana,”  Meya wa Ridgecrest, Peggy Breeden  aliliambia shirika la habari la  Reuters.

BBC/AFP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles