24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

CAG kuifuata IPTL Oman

Zitto Kabwe
Zitto Kabwe

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, amesema taarifa alizopewa na Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), hadi sasa ni muhusika mmoja pekee ambaye hajahojiwa juu ya uchotwaji wa mabilioni ya fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Amesema kwa sasa kazi itakayofanywa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ni kufanya mahojiano na mmoja wa wahusika, Mkurugenzi wa Piper Link atakayefuatwa nchini Oman ili kukamisha ripoti,” alisema Zitto.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Zitto alisema hadi sasa hatua za uchunguzi kuhusu sakata hilo linakaribia kukamilika na ripoti inatarajiwa kuwasilishwa bungeni Novemba 4, mwaka huu.

“Hadi sasa suala hili linakwenda vizuri na ninachowaomba Watanzania wawe na subira kwani baada ya ripoti ya uchunguzi kukabidhiwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kila muhusika atakayekuwa ametajwa katika ripoti ataitwa na kuhojiwa mbele ya umma.

“Kama ujuavyo kuwa suala hili lina mslahi kwa taifa nasi PAC hatutoficha taarifa hata chembe na kila hatua itakuwa  ikishuhudiwa na waandishi wa habari. Na hivi sasa tunaamini ndani ya kipindi kifupi Mkurugenzi wa Piper Link atafuatwa nchini Oman ili kukamilisha ripoti ya CAG.

“Nasi baada ya kukabidhiwa kwa mujibu wa utaratibu tutawahoji wahusika na kisha kuiwasilisha taarifa kwa Spika wa Bunge kwa hatua zaidi,” alisema

“Sisi Kamati ya PAC kwa niaba ya Bunge ndio tuliomba uchunguzi wa suala hili na pindi itakapokamilika tutaeleza kwa uwazi na Watanzania wasiwe na hofu kila kilichomo ndani taarifa ya CAG watakifahamu, tutaisambaza kwao,” alisema Zitto.

Sakata la Akaunti ya Escrow lilibuka kutokana na kile kinachoelezwa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) kulalamika kuwa capacity charge (taarifu) wanayolipa kwa IPTL ni kubwa.

Zitto alisema pamoja na uchunguzi unaoendelea, lakini hawezi kuzungumzia upande wa Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwani ni chombo chenye mamlaka yake kwa mujibu wa sheria.

Taarifa ya CAG

Wakati Zitto akisema hayo, taarifa ya CAG kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, inasema ukaguzi huo haujakamilika kwa muda uliopangwa na kwamba bado unaendelea kwa kuzingatia hadidu za rejea.

Aidha taarifa hiyo ya ofisi ya CAG inasema ukaguzi huo uliombwa na ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Madini na Nishati.

“Ukaguzi wa akaunti ya Tegeta Escrow uliombwa na Katibu wa Bunge na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini. Ukaguzi huu unalenga kufanya uchunguzi wa kina ambao utatoa taarifa kamili yenye kuonyesha hali halisi kuhusu miamala (transactions) kwenye akaunti maalumu ya Tegeta Escrow kisha kutoa taarifa kuhusu ukaguzi huo.

“Kwa kuwa hadidu za rejea pekee haziwezi kuonyesha ukubwa wa kazi bali utekelezaji wa kazi yenyewe ndio unaoweza kutoa taswira halisi, ni vyema umma wa Watanzania ukatambua kuwa ukaguzi huu haujaweza kukamilika kwa kipindi kilichokadiriwa awali, hivyo unaendelea kwa kuzingatia hadidu za rejea na kifungu cha 29 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya mwaka 2008,” inasema taarifa hiyo.

Inaeleza kuwa ongezeko la muda wa kukamilisha ukaguzi huo limetokana na uhitaji wa kukusanya maelezo yanayoendana na vielelezo vinavyojitosheleza ili kumsaidia mkaguzi kufikia malengo ya ukaguzi huo.

Kwamba ukusanyaji wa taarifa hizo unategemea wahusika kutoka taasisi za Serikali, mashirika ya umma  na watu binafsi waliopo ndani na nje ya nchi.

“Licha ya changamoto zilizoainishwa hapo juu, ukaguzi wa IPTL unaendelea na mwelekeo ni mzuri kwa sababu ni maeneo machache tu yaliyobakia ambapo yatakapokamilika tutawasilisha ripoti kwa taasisi zilizouomba ukaguzi huu kwa mujibu wa sheria.

“Tunaendelea kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa wadau wa ukaguzi huo. Ifahamike kuwa ukaguzi bado unaendelea, hivyo itakuwa ni kinyume na utaratibu kwa ofisi hii kuzungumzia kwa kina taarifa ya ukaguzi wa IPTL kwa sasa.

“Ofisi hii itaendelea kutekeleza majukumu yake yote kwa kuzingatia misingi ya uwazi na uwajibikaji usiokiuka taratibu za kisheria katika kukusanya na kutumia rasilimali za umma,” inasema taarifa hiyo.

MWANZO WA SAKATA

Kwa mujibu wa taarifa za ndani zinaeleza kuwa IPTL ilikuwa inamilikiwa kwa ubia na Kampuni ya VIP Engineering and Management iliyokuwa na asilimia 30 za hisa na Mechmar ya Malaysia iliyokuwa na asilimia 70.

Inadaiwa kuwa, Piper Link Investments Ltd ilinunua hisa asilimia 70 za Mechmar kwa Sh milioni 6 Septemba 2013 na majuma matatu baadaye waliziuza kwa PAP kwa dola za Marekani 300,000  sawa na Sh milioni 500.

Asilimia 30 za hisa zilizosalia ambazo zilikuwa zikimilikiwa na VIP, zilinunuliwa pia na PAP kwa dola milioni 75 za Marekani.

Sakata la IPT lilibuliwa kwa mara ya kwanza na vyombo vya habari kabla ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) kuliwasilisha bungeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles