Bushwick Bill afariki dunia

0
288

TEXAS, MAREKANI 

RAPA Richard Shaw, maarufu kwa jina la Bushwick Bill, amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na tatizo la Kongosho.

Msanii huyo raia wa nchini Jamaica, amepoteza maisha huku akiwa na umri wa miaka 52. Kabla ya kifo chake alikuwa anatambulika kwa urahisi kutokana na ulemavu wake.

Bushwick Bill alikuwa na ulemavu wa miguu pamoja na mikono, ambapo viungo hivyo vyote vilikuwa vifupi na kumfanya aonekane mfupi sana akiwa jukwaani.

Mbali na kuzaliwa nchini Jamaica, lakini alikuwa anaishi nchini Marakeni kwa kipindi chote cha maisha yake ya muziki. Anadaiwa kwamba alikuwa na urefu wa futi 3 na inchi 8.

Kwa mujibu wa TMZ, msanii huyo alianza kugundulika kuwa na tatizo la Kongosho Februari mwaka huu na kudaiwa kuwa ugonjwa wake umefikia hatua ya nne.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here