24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Buriani mradi wa Liganga na Mchuchuma

Mwandishi Wetu

ULE msemo kuwa chelewa chelewa utamkuta  mwana si wako  umejidhihirisha wazi kwenye suala lauwekezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Njombe ambapo mwekezaji, Sichuan Hongda  Group yuko njia panda kwa kukosa mwelekeo na kuungwa mkono.

Kampuni imesema madai yote yalikuwa na haki ya kujadiliwa kikamilifu na Serikali ambayo ilikwisha kutoa vyeti vya vibali vya madini na vishawishi vya uwekezaji.

Sichuan Hongada Group inadai mradi umekuwa ukicheleweshwa na Serikali kutofanya yanayostahili huku ikijisahau  kuwa kampuni hiyo imekuwa ikibadilisha  masharti yake kama vile haijui nini inatakakwenye mradi.

Wachunguzi wa mambo wanasema mradi huo kwa kila hali umepitwa na wakati kwani sheria zimebadilika na masharti yauchimbaji madini yameathiriwa kwa kiasi kikubwa na sheria mpya za Tanzania ambazo zimebadilika kudai kupata faida kwenyeutajiri wake.

Hongda Group inashauriwa nayo kubadilika ilikuzuia isijikute nje ya mradi kwani wanaohitaji mradi huowanazidi kuongezeka.

Muda mwingi umepotezwa na badilika badilika  yake na dhana ya mradi ambayo sasa maudhui ya kisheria yanatoa madai mengi kutokana na Sheria ya Mali ya Taifa ya mwaka 2017 na vile vile Sheria ya Madini 2010 kwa hiyo kwa kiasi kikubwa wataalamu wa Serikali wanadai wa  kulaumiwa  ni kampuni yenyewe na si Serikali.

“Ieleweke wazi kuwa  ukiona majadiliano yanachukua zaidi ya miaka10 ujue jambo hilo haliwezekani na hivyo kuliacha au kutafuta njia nyingine zautekelezaji kwani hakuna mradi duniani unaomalizwa mara moja ila hujadiliwa kutokana  na matatizo yanayojitokezakwani hakuna mtu mwenye nia nzuri kukataa  ukweli unaojitokeza kwani wakati wautekelezaji pande hizo mbili, Serikali na mwekezaji huwa ni wabia  na hivyo huwezeshana ili kufanikisha malengowaliyojiwekea.

Kwa sheria mpya inawataka wawekezaji kutoa asilimia 16 ya hisa bure kwa Serikali.

Aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Dk. Chrisant Majiyatanga  Mzindakaya, ameumia sana  kusikia kuwa mradi huo si kipaumbele tena kwani alipigania sana kuhakikisha unakuwa hivyo. Alipotoka tu watu wameamua kuubwaga mradi bila kutoa sababu.

Wengi niliowauliza nao vile vile wananiuliza wanasema tatizo ni mradi au Wachina? Kwa sababu si vema kuachia dola bilioni 3 ambazo zingeiweka nchi kwenye ramani  ya dunia na hivyo kukosa kila kitu.
Kampuni hiyo ya Sichuan Hongda Group, kampuni  mzazi katika mradi ilishinda zabuni kwa mradi  huo mkubwa sana wa uchimbaji madini na ujenzi tangamano wa  viwanda vya  chuma na makaa ya mawe na usafiri wa reli  hadi  bandari ya Mtwara.

Mradi ulionesha uwezo wa kuunda kazi 5,000 za moja kwa moja na nyinginezo 30,000 zisizo kuwa za moja kwa moja katika mwaka 2010.
Kampuni ya Kichina ilipewa  zabuni ya kuendeleza kwa dola bilioni 3 (Sh trilioni 6.8)  wa chuma lakini sasa unaonekana si kipaumbele  na hivyo Hongda inaona  kuwa  haikutendewa haki.

Serikali  kwa mazingira ya sasa  inaona kuwa kampuni hiyo  ni kiwingu  kwa kuzuia wawekezaji wengine kuingia  kwenye eneo la mradi  na kufanya  wanayotaka kufanya  baada ya kuona  hakuna maendeleo ya haja kwenye mradi huo.

Kuanguka bei ya chuma

Isitoshe wakati fulani kampuni hiyo ilisema kuzalisha chuma wakati huu hakulipi na hivyo walikuwa wanasubiri bei ipande na hivyo madai ya kukosa motisha inaonekana kuwa ni mwendelezo wa kutaka dezo.

Kimsingi katika mazingira yaliyopo si rahisi kuibana Serikali ingawa matendo ya  Waziri wa Fedha, Dk. Phillip Mpango, kuutoa kwenye kipaumbele inahitaji maelezo ya kina.

Isitoshe Hongda Group  inadai uzinduzi wake mradi umejaa ucheleweshaji  usioeleweka na kujaa  sintofahamu na sasa  kukosa msukumo wa  kisiasa.

Hata reli yake imepitwa na ujenzi wa reli ya SGR kwenda Mwanza na nyingine kwenda Kigoma hadi Burundi na Rwanda. Mahitaji halisi yamebadilika ndani ya miaka mitatu.
“Kama mwekezaji mkubwa na alitumia rasilimali nyingi katika maendeleo na utekelezaji wa mradi, Sichuan Hongda, bado ana nia ya kutekeleza mradi huu licha ya changamoto za mara kwa mara ndani na nje ya nchi,” inasema taarifa ya Hongda.

Mchuchuma inadaiwa kuwa na tani milioni 428 za makaa ya mawe wakati Liganga ina tani milioni 128 za chuma na kampuni ya Kichina imetoa mpango jumuishi wa madini na uzalishaji umeme  MW 600.

Makampuni hayo yatatengeneza madini yote ndani ya nchi ili kutenganisha titani na vanadium kutoka kwa madini ya chuma.
Wizara ya Fedha hakupatikana kusema kwanini haijasaini  utekelezaji wa mradi huo kwa kutoa  motisha kwa muda mrefu licha ya ahadi ya mwaka jana ya aliyekuwa Waziri wa Biashara na  Uwekezaji, Charles Mwijage, kudai ilikuwa inasubiriwa saini ya Rais Magufuli tu.

Suala la Waziri wa Fedha, Dk. Phillip Mpango, kuunyang’anya mradi nguvu ya kisiasa, linadai maelezo ya kina kwani suala hilo limeanza kuleta joto la kisiasa nchini na wadau wa uchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles