26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Buriani Dk. Mselly, umeondoka na ndoto zako – 2

NA SARAH M. KASSIM

WIKI iliyopita tulichapisha sehemu ya kwanza ya mahojiano kati ya, Dk. Mselly na Mwandishi wa gazeti hili yaliyofanyika Novemba, 2016, nyumbani kwa Dk. Mselly katika Mji wa Kalstard nchini Sweden. Mahojiana haya yana lengo la kukumbuka juhudi kubwa za Mtaalamu huyu katika utengenezaji bidhaa za chuma aliyefariki dunia Septemba 10,2018.

Dk. Mselly ni miongoni mwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi wenye uchu wa kusaidia Watanzania wenzao katika nyanja mbalimbali lakini wamekuwa wakikwamishwa na sababu ambazo haziko wazi.Katika sehemu ya kwanza ya mahojiano na Dk. Mselly alieleza ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuwekeza katika elimu na kwa maneno yake aliona kuwekeza upande wa elimu ni kitu cha maana zaidi kuliko kwenda kujenga vitu vya ajabu. Endelea na sehemu ya pili ya makala haya….

MTANZANIA: Kwa maoni yako unafikiri ni kwanini nchi yetu inakwama katika baadhi ya mambo?

Dk. MSELLY: Kuna vitu viwili ambavyo vinafanya nchi yetu isiendelee, cha kwanza sisi Watanzania tulikuwa hatujui kama tunaibiwa, katika misitu,tulikuwa hatujui kama pale kuna mali inakwenda na katika madini, sasa ukishaanza kufukua na wananchi wakagundua kama walikalia utajiri, utakwamishwa. Kwahiyo utaona namna nilivyojitolea na mimi naamini elimu yangu ndio muhimu zaidi katika kuwanyanyua Watanzania wenzangu.

 

MTANZANIA: Moja ya kilio chaDiaspora ni kukwamishwa pale wanaporudi nyumbani kutaka kuwekeza au wanachukuliwa ni kama vile wageni kabisa katika nchi yao mama, hili wewe unalionaje?

  1. MSELLY: Tufanye kama Rwanda, alichofanya Kagame

kwamba Mnyarwanda yeye anayeishi nje akitaka kurudi na arudi ajenge nchi na mawazo yao yanakaribishwa, ndio maana ile nchi katika muda mfupi tu ikabadilika, lakini sisi tulioko nje tunachezewa tu. Mimi niliwahi kuwa Mwenyekiti wa Mazingira Sweden yote na ukiona Mswidi amekupa kazi hiyo ujue amekuamini.. Waswidi wananiamini, lakini Watanzania hawataki kuniamini. Mimi kila baada ya miezi miwili pale kazini kwangu napelekwa nje ya nchi kuzungumzia utaalamu wangu.

MTANZANIA: Unaionaje hii kauli ya Rais kwamba anataka Tanzania iwe ya uchumi wa viwanda?

  1. MSELLY: Kama alivyosema Rais, Kama kweli tunataka kuwa nchi ya viwanda lazima tuwe serious katika hili, kwanza kile kiwanda cha chuma tujue kwamba kinataka kufanya nini, tunaamua kutengeneza Construction Steel au kiwanda cha kutengenezea masufuria, ni lazima Serikali ijue hilo, au tunataka tuuze kama raw materials

ambayo Wachina ndio wanaifuata kwa sababu wameshajua sisi hatujui na kama mtu hujui wanakudanganya wanachukua, sio wajinga wale.

Mimi nafikiria kwamba jambo la muhimu ni kwamba Serikali iwe serious na hakuna mtu mwingine ambaye anaweza akafanya hiyo kazi kama sio Serikali. Serikali tu iipe kipaumbele kama proudly of a country wajue kama chuma ndio kinaendesha jeshi na ndio kitu cha maana. Na sio kama nasema kwa ajili ya utaalamu wangu.

MTANZANIA: Kwa kipindi cha miaka fulani Tanzania ilikumbwa na kashfa ya baadhi ya watu kuuza vifaa vya ujenzi visivyo na ubora hususani nondo na kusababisha baadhi ya majengo kuanguka, unafikiri tulikosea wapi kama Taifa?

  1. MSELLY: Ndio kile nilichosema kwamba kama Taifa kuwe na maabara na Shirika la Viwango (TBS), liwe na wataalmu wa kuangalia kwamba kitu hakiendi, pengine haina wataalamu wazuri na kama wapo basi wanapewa hiyo dili.

Mimi nilifika pale, ukishavunja nondo kwa mkono ujue hicho ni kitu kichafu, huwezi kuamini, nondo inavunjika, liliposhuka jengo pale katikati ya Jiji la Dar es Salaam, mimi nilifika kwa yule Muhindi na hata kule VETA Arusha nilipofika niliona hawana maabara.

Kwa mfano ule mchanga wote pale bandarini ile ni malighafi unaweza kutengeneza glasi, lakini hakuna

maabara ya kupima. Kwa hiyo mimi mawazo yangu ndio

hayo ni kwamba I think ni lazima tu re-think about our strategy, tusiseme tu ili kupata kura, ni lazima tuangalie strategy zetu, Je, zinakwendaje? Kwa mfano tuangalie watu muhimu kwa mfano hata mimi usiponilipa, tiketi ni kitu kidogo sana, kama Serikali inaniambia Dk. Mselly kuna kitu cha haraka sana tunataka utupe mawazo haya.

Usiwe unatoa uamuzi wa vitu ambavyo uwezo huna, Unakaa na Wachina unadiscuss kuhusu chuma wakati hata siku moja hujafanya utafiti wa chuma kujua Wha is it? Ni muhimu kuwatumia Diaspora wenye utaalamu, ndio maana nilisema ile Data Base iliyoanzishwa ni muhimu sana, ni lazima itumike, sio imeanzishwa tu na itumike kwamba kama kuna utaalamu unatakiwa basi tuwajue wapi walipo wataalamu wetu duniani kote. Ofisi za ubalozi zitumike kuwatambua wataalamu hao na kuwaomba wataalamu wajitokeza, tuwe wazi katika hili.

Lakini kama hatuendi hivyo its over, sasa kwanini walinituma mimi nikasome Bulgaria, walinituma nikacheze? Rais wetu kama anao uwezo inatakiwa nchi iweke priority. Kama si hivyo hatutofika mbali.

Kwa hiyo mimi mawazo yangu ndio hayo ni

kwamba I think ni lazima tu re-think about our

strategy, tusiseme tu ili kupata kura, ni lazima

tuangalie strategy zetu, Je, zinakwendaje?

Buriani Dk. Mselly Mbwambo Nzota  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles