27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

BUNGE LA ULAYA LAIJADILI KENYA

STRASBOURG, UFARANSA


BUNGE la Ulaya jana lilitarajia kuijadili Kenya, siku chache tu baada ya jopo lake la waangalizi wa uchaguzi kuchapisha ripoti iliyounanga uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwaka jana.

Bunge linakutana mjini hapa na mjadala kuhusu Kenya ulitarajia kuanza jana saa 11 jioni za Afrika Mashariki.

Mkuu wa jopo hilo, Marietje Schaake, ni miongoni mwa waliotarajia kuhudhuria majadiliano hayo.

Schaake aliweka ujumbe wake katika akaunti yake ya Twitter juzi jioni akisema: “Kesho mchana Bunge la Ulaya litafanya mdahalo kuhusu hali ya nchini Kenya. Nitatoa taarifa kwa muhtasari wakati matokeo ya mjadala yatakapofahamika.”

Wiki iliyopita, Schaake alitupiana maneno na Serikali ya Kenya baada ya kutoa ripoti ya jopo lake mjini Brussels, Ubelgiji badala ya Kenya, ambako anasema yeye na jopo lake hawakutakiwa.

Wakati akidai kuwa Serikali ya Kenya haikuwa tayari kulipokea jopo hilo, Kenya ilisema kutoa ripoti bila kuishirikisha ni makosa na dharau.

Lakini Schaake alisema wakati makubaliano ya tarehe za utoaji ripoti yaliyofikiwa Juni mwaka jana zikikaribia, Serikali haikuonyesha utayari wa kuwapokea na hivyo kuamua kuitoa kwingine.

Balozi wa Kenya nchini Ubelgiji, Johnson Weru, alisema ni Schaake aliyeenda kinyume cha makubaliano.

Rais Uhuru Kenyatta alishinda uchaguzi wa marudio na kutetea urais kwa muhula wa pili baada ya ushindi wake wa awali kufutiliwa mbali na Mahakama ya Juu.

Lakini jopo la waangalizi lilisema Wakenya walikuwa na matumaini makubwa, ambayo hata hivyo yaligeuka kuwa ya kufadhaisha na kuliacha taifa likiwa limegawanyika.

Ripoti hiyo imesema kuwa mchakato wa upigaji kura uliharibiwa na hatua ya viongozi kuzishambulia taasisi huru na kutofanyika kwa mazungumzo baina ya pande mbili hasimu, jambo lililochangia kuenea mizozo na machafuko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles