27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

BOTI YAPOTEA ZIWANI NA WATU SITA

Na Editha Karlo-Kigoma

BOTI ya mizigo iliyokuwa ikitokea Kigoma kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo eneo la  Kalemi imepotea katika ziwa Tanganyika ikiwa na watu sita.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdnand Mtui, alisema boti hiyo ilikuwa na shehena ya vitunguu maji magunia 110, ngano mifuko180, mafuta ya taa dumu 20 na kreti 70 za soda ambayo mpaka sasa haijulikani ilipo.

Mtui alisema tukio la kupotelea ziwani boti hiyo limetokea Januari 23 mwaka huu,  saa 16:30 jioni, ambapo boti hiyo iliondoka katika bandari ndogo ya Kibirizi ikiwa na shehena hiyo ya mizigo lakini mpaka sasa haijafika Kongo na haijulikani ilipo na hakuna kilichopatikana kati ya mizigo wala abiria waliokuwa kwenye boti hiyo.

Askari wanamaji wakishirikiana na Chama cha Wamiliki wa Maboti wanaendelea na utaratibu wa kuitafuta boti hiyo, inasemekana imepotelea katika maji yaliyopo Kongo.

Mtui alisema kumekuwa na taarifa zilizo kuwa zikizungumzwa mitaani kwamba  kuna miili imeonekana, taarifa hizo si za kweli hadi sasa hawajajua kama watu hao watakuwa hai au wamekufa maji.

"Tumewasiliana na watu walio pembezoni mwa Ziwa Tanganyika hawajaona kitu chochote hadi sasa, ninawaomba wananchi kuwa na subira wakati jitihada mbalimbali za kutafuta miili inaendelea ili waweze kuitambua,"alisema.

"Baada ya kupata taarifa kuhusu  boti hiyo iliyokuwa ikielekea Kongo kwamba haijafika kwa muda uliotakiwa, Polisi kwa kushirikiana na wamiliki wa maboti walianza jitihada za kulitafuta boti hilo maeneo ya mwambao mwa Ziwa Tanganyika na hatujapata taarifa yoyote.

“ Boti ingekuwa imezama mizigo iliyo kuwemo katika boti hiyo ingekuwa imeanza kuelea, tumewasiliana na  mikoa baadhi ambayo Ziwa Tanganyika limepita pamoja na nchi za Burundi na Kongo kupitia ubalozi mdogo waweze kutujulisha endapo wataiona boti hiyo," alisema Mtui.

Baadhi ya ndugu wa wasafiri walio kuwemo katika boti hiyo wameanza kutandika msiba kuwaombolezea ndugu zao waliopotea katika boti hiyo , Hamisi Kakolwa ni mmoja kati ya abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea Kalemii Kongo.

Mgeni Kakolwa ni mdogo wa Hamis Kakolwa ambaye alisema ndugu yao aliondoka Januari 21 kuelekea Kalemii kupeleka biashara zake, baada ya siku mbili kupita walifanya mawasiliano na watu wa Kongo kujua kama boti waliyokuwa wakisafiria ndugu yao, wakaambiwa haijafika.

Kakolwa alisema familia baada ya kuona hakuna mafanikio ya kuipata boti hiyo kwa siku saba waliamua kuandaa msiba wa kumuombolezea ndugu yao kwasababu hawana uhakika kama atakuwa amepona au amekufa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles