24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Boris Johnson kumrithi Theresa May

London, Uingereza

Boris Johnson amechaguliwa kuwa Kiongozi mpya wa Chama cha Conservative na ndiye atakayekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza akimrithi Theresa May, ameshinda kwa zaidi ya kura 92,000 dhidi ya kura 46,656 alizopata mpinzani wake wa karibu, Jeremy Hunt.

 Johnson ametangazwa leo Jumanne Julai 23, ushindi wake ni sawa na asilimia 66. 4 ya kura zote zilizopigwa ambazo ni chache kuliko alizoshinda David Cameroon mwaka 2005 aliyeshinda kwa asilimia 67.6 ya kura zote zilizopigwa mwaka huo.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Meya huyo wa zamani wa Londoni amesema Uingereza itajitoa katika Umoja wa Ulaya (Brexit), ifikapo Oktoba 31 mwaka huu.

“Ni heshima kubwa kwangu kuchaguliwa na kupewa kipaumbele kuwa Kiongozi wa chama change, nadhani mnajua tunaweza kujitoa Brexit na watu wa nchi hii wametuamini kuwa tunaweza kufanya hivyo na tunaenda kufanya hivyo sasa,” amesema Johnson.

Johnson amekuwa akizungumza mara kwa mara katika kampeni zake kuwa kipaumbele chake ni Uingereza kujitoa Brexit sakata ambalo lilipelekea Waziri Mkuu anayeondoka madarakani May kutangaza kujiuzulu.

Waziri Mkuu huyi mpya wa Uingereza atakabidhiwa ofisi kesho Jumatano Julai 24, na Waziri Mkuu anayeondoka madarakani May, baada ya kutoa hotuba yake ya mwisho katika bunge la nchi hiyo.

Muda mfupi baada ya Johnson kutangazwa, Rais wa Marekani Donald Trump amemtumia salamu za pongezi kwa kushindi huo ambapo amemuandikia ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter usemao; “Pongezi kwa Boris Johnson kwa kuwa Waziri Mkuu Uingereza, atakuwa bora.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles