Bondia Mwakinyo awasili Kenya

0
462

MWANDISHI WETU

BONDIA nyota wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, amewasili jijini Nairobi, Kenya tayari kwa pambano lake la kimataifa dhidi ya bondia kutoka Argentina, Eduardo Gonzalez, lililopangwa kufanyika Machi 23 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta.

Mwakinyo alikuwa anafundishwa na kocha Muingereza, Tony Bellew akiwa kambini jijini Liverpool, England chini ya ufadhili wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa.

Mbali na Mwakinyo, Bellew anamfundisha bondia wa kike, Fatuma Zarika, ambaye atapambana na Catherine Phiri wa Zambia katika pambamo la Ubingwa wa Dunia wa uzito wa Super Bantamweight wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC).

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas, alisema mabondia hao wamepata mafunzo bora na ya kisasa kutokana na umuhimu wa pambano hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here