23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bodi ya wadhamini yapigilia msumari CUF

Profesa Lipumba
Profesa Lipumba

Na Muhamed Khamis (UoI), ZANZIBAR

BODI ya udhamini ya Chama cha Wananchi (CUF),  imesema haimtambui Profesa Ibrahim Lipumba kama mwenyekiti wa chama hicho.

Imesema pia kwamba haimtambui kama mwanachama wa kawaida hasa baada ya kufukuzwa rasmi uanachama  na Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho.

Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini  CUF, Abdallah Khatau alipozungumza na waandishi wa habari  mjini Unguja jana.

Alisema   bodi hiyo imepuuza wito wa Profesa Lipumba alioutangaza kutaka kuitishwa   kikao cha wajumbe wa bodi ya udhamini kwa vile  hana mamlaka hayo kwa mujibu wa katiba ya CUF.

“Lipumba kwa sasa si mwenyekiti tena wa CUF na pia si mwanachama wa CUF baada ya kufukuzwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa hivyo tumeamua kupuzia wito wake aliotoa jana (juzi),’’alisema Khatau.

Alisema bodi ya uadhamini ya chama hicho itaendelea kuwajibika kwa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama kama inavyotakiwa na Ibara ya 98(5) ya katiba ya chama ambalo ndilo linaloiteua bodi na litaheshimu uamuzi wote  utakaofikiwa.

Alisema bodi   itahakikisha  inachukua hatua za sheria kwa mujibu wa uwezo wake iliopewa na Ibara ya 98(3) na 98(4) kurejesha chini ya dhamana yake mali zote za chama zilizovamiwa, kuporwa na kuhodhiwa na Profesa Lipumba na aliloliita genge lake likiwamo jengo la Ofisi Kuu ya chama hicho lililopo Buguruni  Dar es Salaam.

Alisema  bodi hiyo itachukua hatua za  sheria kwa uwezo wake iliopewa na Ibara ya 98(4) dhidi ya Ibrahim Lipumba kwa kumtaka alipe gharama na hasara zote alizozisababisha kwa kuvamia Mkutano Mkuu Maalumu wa Taifa wa chama uliofanyika Agosti 21, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles