24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bobi Wine: Rais Museveni mbaya kuliko Idi Amin

KAMPALA, UGANDA

MBUNGE machachari wa upinzani ambaye pia ni mwanamuziki, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, amemwelezea Rais Yoweri Museveni kuwa mlevi wa madaraka.

Bobi Wine alienda mbali zaidi akidai Museveni ni mtu mbaya kuliko dikteta wa zamani wa nchi hii, Idi Amin Dada, ambaye analaumiwa kwa uchinjaji wa Waganda wengi wakati akiwa madarakani kuanzia mwaka 1971 hadi 1979.

Katika mahojiano na televisheni ya Citizen juzi usiku, mwanamuziki huyo aliyegeukia siasa, alisema anaamini Museveni ameharibiwa na waliomzunguka kwa vile wanammwagia sifa za kijinga zinazompotosha.

Kwa mujibu wa Bobi Wine, taasisi na uongozi wa nchi umemshinda Museveni kwa sababu watu waliomzunguka ni ndugu zake na kutoka kabila lake.

“Imeelezwa kuwa madaraka hupofusha, ninaamini amelewa madaraka. Ameaminishwa na waliomzunguka, ambao wananufaika na uwapo wake kuwa yu Mungu mdogo,” alisema Bobi Wine.

Na alipoulizwa na mtangazaji maarufu Jeff Koinange wakati wa mahojiano hayo ya moja kwa moja na kituo hicho cha televisheni cha Kenya juu ya ushauri ambao angempatia, alisema Rais Museveni awe mkweli kwa maneno yake na watu.

Lakini pia mtunga sheria huyo alieleza matumaini yake kuwa hali itabadilika kwa vile Museveni hatobakia madarakani milele.

“Uhuru huja kwa wale wanaoupigania, si hao wanaolia. Kwa kadiri unavyolia, ndivyo watu zaidi wanavyokufa. Hivyo inuka na linda haki zako,” alisema Bobi Wine.

Agosti mwaka huu, Bob Wine alituhumiwa na utawala wa Museveni kuushambulia msafara wake huko Arua, kitu kilichoshuhudia machafuko yaliyosababisha kukamatwa na kushikiliwa kwake.

Alisafiri kwenda Marekani kwa matibabu maalumu baada ya mateso aliyopata wakati akiwa jela kabla hajarudi hivi karibuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles