Bobi Wine awashukuru Wakenya

0
912

KAMPALA, UGANDA

NYOTA wa muziki nchini Uganda ambaye pia ni mbunge, Robert Ssentamu anayejulikana kwa jina la Bobi Wine, ametuma ujumbe kwa mashabiki wake nchini Kenya kutokana na mchango wao wa kumfanya awe huru.

Msanii huyo aliwekwa ndani mwezi uliopita kutokana na kusababisha vurugu katika masuala ya kisiasa, hata hivyo kwenye vurugu hizo zilisababisha gari ya Rais Yoweri Museveni kuvunjwa kioo.

Msanii huyo amewashukuru mashabiki zake nchini Uganda lakini amedai hawezi kuwasahau mashabiki nchini Kenya kwa kuwa waliungana kuhakikisha anakuwa huru.

“Nitumie nafasi hii kuwashukuru mashabiki zangu wote ambao wanaongea Kiswahili barani Afrika, lakini mashabiki zangu nchini Kenya walipambana kwa kiasi kikubwa ili niweze kuwa huru, ninawashukuru sana kwa sapoti yao.

“Nilikuwa napokea jumbe mbalimbali kutoka Kenya, ninawaahidi kwamba nitapanga siku ya kukutana ili tuweze kuimba pamoja wimbo kwa ajili ya uhuru,” alisema msanii huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here