24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Bobi Wine amjulia hali aliyeteswa naye

NAIROBI, Kenya

MBUNGE wa Uganda, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, juzi aliwasili katika Hospitali ya Aga Khan iliyopo mjini hapa alikolazwa mmoja wafuasi wake waliokamatwa na kuteswa siku moja kabla ya uchaguzi wa marudio wa Jimbo la  Arua.

Akizungumza kupitia ujumbe alioutuma kwa njia ya mtandao wake wa kijamii wa Twitter, Bobi Wine ambaye kwa sasa yupo jijini hapa, alisema kwamba Sauda Madada, bado anaendelea kupata nafuu baada ya kupewa rufaa kutoka Kampala kuja hapa ili kupatiwa matibabu bora.

“Dada yetu mpambanaji Sauda Madada bado anaendelea kuuguzwa katika Hospitali ya Aga Khan, Nairobi. Kipigo alichokipata katika Jimbo la Arua kilimuacha katika hali mbaya na ndiyo maana akapewa rufaa ya kuja mahali hapa.

“Shukrani nyingi ziwaendee madaktari wote waliomuhudumia tangu awasili hapa. Shukrani sana na yeye anawasalimia,” aliondika Bobi Wine kupitia mtandao wake wa Twitter.

Kabla ya kuwasili hospitalini hapo, Bobi Wine ambaye alikuwa ameambatana na Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, walihutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Kibera ambako aliwataka Wakenya kumuunga mkono ili aweze kushinda vita ya uhuru nchini  Uganda.

“Sipo hapa kuomba bunduki bali nipo mahali hapa kuwaomba kuendeleza undugu na umoja ili kupambana na vitendo vya unyanyasaji katika nchi yetu wakati tunapozungumza kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki isiwe ni klabu ya marais bali ni kuhusu uananchi wetu.

“Babu zetu walipambana kwa ajili ya uhuru na ukombozi, waliahidi kukomesha ukoloni, lakini sasa mambo yamebadilika kutoka ukoloni wa kizungu hadi wa mtu mweusi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles