23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bobi Wine akimbilia mafichoni kukwepa polisi

KAMPALA, UGANDA

MBUNGE wa upinzani nchini hapa, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, amelazimika kukimbilia mafichoni baada yakufanikiwa kuwakimbia polisi waliovamia hotelini alipokuwa amefikia mjini Jinja.

Kwa mujibu wa wakili wake, Robert Amsterdam, mbunge huyo alikuwa akiajiandaa kutumbuiza katika tamasha ambalo lilipangwa kufanyikausiku wa kuamkia jana katika mji huo wa Jinja uliopo umbali wa kilometa 80 masharikimwa Kampala.

Hata hivyo wakili huyo alisema jana kwamba kabla ya kufanyika tamasha hilo, polisi walivamia hotelini kwake jambo ambalo lilimlazimisha mbunge huyo wa Kyaddondo Mashariki kukimbilia mafichoni.

“Kyagulanyi alilazimika kutafuta hifadhi baada ya polisi kuvamia hotelini kwake usiku na inavyoonekana washirika na wafuasi wake walikamatwa na wengine kupigwa,” ilieleza taarifa ya wakili huyo mwenye makazi yake jijini London nchini Uingereza.

Kwa upande wake mbunge huyo usiku wa kuamkia jana aliandika katika ukurasa wake wa  Twitterakieleza kuwa polisi wanawashikilia baadhi ya wafuasi wake.

“Polisi usiku wa leo (juzi) wamevamia katika hoteli ambayo tulikuwa tumepumzika mimi na wenzangu kabla ya kwenda kwenye tamasha, wamewakamata wafuasi wangu na ninavyozungumza wametanda katika maeneo ya karibu na hoteli wakinifuta.

“Wamewapiga baadhi yao, wamewakamata na kuwapakia kwenye gari lao na kuondoka nao mahali pasipojulika bila ya kuwa nakosa lolote,” aliandika.

 Wakili Amsterdam aliuita uvamizi huo ni mkakati wa wazi uliopangwa na vyombo vya dola vya Uganda ambavyo vinakiuka haki za  Bobi Wine na akasema kuwa tamasha hilo lilikuwa limeruhusiwa na akahoji ni kwanini wanamuziki wengine hawakukamatwa.

Bobi Wine ni miongoni mwa watu mashuhuri nchini hapa ambao wamekuwa wakimkosoa kiongozi wa muda mrefu Rais Yoweri Museveni na Serikali yake jambo ambalo limesababisha kukatazwa kutumbuiza hadharani.

Tamasha lake la mwezi uliopita liliruhusiwa baada ya kukubaliana na polisi kuwa halitakuwa la kisiasa kutokana na kwamba nyimbo zake nyingi zinaelezea matatizo ya kijamii na zinamtaka Rais  Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa mudawa miaka  32 astaafu.

Mwezi Agosti mwaka huu, Bobi Wine alifunguliwa mashtaka ya uhaini sambamba na wanasiasa zaidi ya  30  wakidaiwa kurushia mawe msafara wa Rais  Museveni baada ya kumalizika mkutano wa kampeni katika mji wa Arua uliopi Kaskazini Magharibi mwa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles