22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Binti mwenye kidonda aanza matibabu Muhimbili

Tunu Nassor, Dar es Salaam

Hatimaye Mariam Rajab (25), mkazi wa Singida anayesumbuliwa na kidonda mgongoni, amepokewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.

Mariam ambaye video yake ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii akiomba msaada wa matibabu, amewasili hospitalini hapo saa sita usiku wa kuamkia leo Aprili 18.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Ofisa Habari wa MNH, John Steven amesema  Mariam amepokelewa katika Idara ya Magonjwa ya Dharura.

“Mgonjwa tumempokea katika Idara ya Dharura  ambapo amelazwa huku akiendelea kufanyiwa vipimo vya awali ili aweze kuonana na jopo la madaktari bingwa wa upasuaji kwa ajili ya kupatiwa matatibu zaidi,” amesema Steven.

Amesema Mariam ameletwa na gari la wagonjwa (Ambulance) kutoka Singida ambapo safari yake ilianza jana saa 8:00 mchana.

Katika ujumbe wa video ulikuwa ukisambaa ulimuonesha Mariamu akiomba msaada wa kupatiwa matibabu ya kidonda kinachomsumbua.

“Mimi naitwa Mariam Rajabu naishi katika Mkoa wa Singida, Mtaa wa Mnung’una naishi katika familia ya kimasikini, wazazi wangu hawana uwezo wa kunisaidia tatizo langu, tatizo lenyewe ambalo ninalo ni kidonda ambacho kipo hapa mgongoni, naombeni Watanzania wenzangu muweze kunisaidia niweze kwenda Hospitali ya Muhimbili ili niweze kupata matibabu. Sina cha kuwalipa bali Mungu atawalipa, asanteni,” amesema Mariam katika ujumbe wa video.

Kutokana na taarifa hiyo, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu aliuagiza Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kumtafuta Mariam ili apelekwe hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles