27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Binti anayeugua kidonda ahamishiwa Ocean Road

CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAAM

BINTI wa Singida aliyepelekwa  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akisumbuliwa na kidonda mgongoni, Mariam Rajab amehamishiwa Hospitali ya Saratani, Ocean Road kwa uchunguzi zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya MNH) wakati akitoa ripoti ya uchunguzi wa awali wa afya ya Mariam, Dar es Salaam jana, Daktari Bingwa wa Upasuaji, Dk. Mkoma alisema mgonjwa huyo  amekwisha kufanyiwa vipimo mbalimbali   na kubaini ugonjwa wake.

“Uchunguzi wetu wa awali tumejiridhisha ugonjwa wa Mariam hivyo leo (kesho) atahamishiwa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road kwa ajili ya uchunguzi wa vipimo mbalimbali,” alisema Mkoma.

Hata hivyo hakuwa tayari kuelezea matokeo ya awali waliyobaini kuhusu ugonjwa wa Mariam na badala yake alisisitiza kuwa ugonjwa na majibu ya vipimo vya mgonjwa ni siri ya daktari na mgonjwa.

Alisema ana imani baada ya mgonjwa huyo kufanyiwa vipimo Ocean Road atarejeshwa tena Muhimbili ili jopo la madaktari bingwa waweze kuendelea na uchunguzi mwingine.

  Dk. Mkoma ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Upasuaji MNH aliitaka jamii kuwa makini na makovu kwa kuwa asilimia kubwa yanayorudia vidonda husababisha saratani.

Alisema ni vema jamii ijenge mazoea ya kufanya vipimo vya afya   na kuchunguza makovu mwilini mwao.

 Alisema uchunguzi wa makovu mengi yanayorudia vidonda matokeo ya vipimo vyake huwa ni saratani.

Naye Mariam alisema kwa sasa ana matumaini ya kupona baada ya kupokewa katika hospitali hiyo na kufanyiwa vipimo mbalimbali.

Alisisitiza kuwa asingependa kuelezea zaidi juu ya ugonjwa wake ambao alisema ulianza kama jipu.

Mariam alipokelewa Muhimbili Aprili 18, mwaka huu akitokea mkoani Singida na  tayari amefanyiwa vipimo mbalimbali vya damu, sehemu ya maabara, kidonda, kichwa na kifua.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles