30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

BILL GATES KUMWAGA MABILIONI NCHINI

TAASISI ya Bill na Mellinda Gates imetenga Sh bilioni 777.084 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali nchini ikiwamo sekta ya afya.

Mwenyekiti Mwenza wa taasisi hiyo ambaye pia ni tajiri namba mbili duniani, ametoa kauli hiyo leo Agosti 10, Ikulu jijini Dar es Salaam katika mazungumzo na Rais Dk. John Magufuli.

Ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na sekta ya kilimo, afya na mifumo ya kielektroniki ya upatikanaji wa taarifa.

Gates ambaye pia ni mmiliki wa kampuni za Microsoft na Cascade Investement LLC, amesema kama ambavyo taasisi yake imeshirikiana na Tanzania katika kuimarisha huduma za afya hapa nchini, fedha hizo zitaelekezwa zaidi katika utekelezaji wa miradi ya afya.

“Tutaelekeza fedha hizi zaidi katika kupunguza vifo vya uzazi, kukabiliana na ugonjwa wa malaria, kuimarisha lishe na kukabiliana na utapiamlo, pia zitaelekezwa katika sekta ya kilimo ambako zitasaidia kuongeza uzalishaji wa mazao, kuzalisha mbegu bora na kuboresha ufugaji utakaoongeza chakula na pia zitasaidia kuweka mifumo ya kisasa ya upatikanaji wa taarifa,”amesema.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles