30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Bilioni 7 kujenga Kagera

meja-jenerali-mstaafu-salumNA EDITHA KARLO-KAGERA

ZAIDI ya Sh bilioni 6.7 zinahitajika kwa ajili ya kujenga na kurekebisha makazi ya wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, mwaka huu mkoani Kagera.

Fedha hizo zinahitajika endapo utafikiwa uamuzi wa kutolewa mgao uliopangwa awali wa kila kaya moja kupewa mifuko mitano ya saruji na bati 20.

Tathimini inayoendelea kufanyika, imebaini kuwa nyumba 2,072 zimeanguka kabisa, nyumba 14,525 zimepata nyufa kubwa ambazo hazipaswi kuishi watu, wakati nyumba zaidi ya 9,000 zinahitaji marekebisho.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu alisema hayo jana wakati akitoa taarifa kwa Kamati ya Maafa ya Waziri Mkuu ikiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenester Mhagama.

Alisema takwimu hizo ni za makazi ya wananchi tu na majengo ya taasisi kama vile shule, makanisa, misikiti, vituo vya polisi, zahanati na magereza havijaunganishwa.

“Wataalamu wamesema shule moja kama ile ya Ihungo, ili kuirudisha katika hali yake ya kawaida inahitaji Sh bilioni 4.5.

“Bado tunaendelea kupokea misaada ambapo hadi Septemba 18, mwaka huu vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh milioni tano vimepokelewa na zaidi ya Sh milioni 663 zimeishaingizwa katika akaunti ya maafa,” alisema.

Kijuu alisema harambee iliyofanyika wiki iliyopita ikiongozwa na yeye mwenyewe ilifanikisha kupatikana kwa Sh milioni saba taslimu na ahadi Sh milioni 700.

Wakati huo huo, Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Chirau Mwakwere amekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali ikiwamo mabati 4,000, magodoro 100 na mablanketi 400 kwa niaba ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

“Tunakumbuka kauli ya hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliyotoa kuwa binadamu wote ni ndugu na Afrika ni moja kwa hiyo sisi ni ndugu inabidi tusaidiane kwa shida na raha,” alisema balozi Mwakwere.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles