24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

BILIONI 2.2 KUJENGA SHULE ILIYOUNGUA LINDI

Jumla ya Sh bilioni 2.27 zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Lindi iliyoungua moto mwaka 2016.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa mkoa huo, Godfrey Zambi ameitisha harambee ya kuchangisha fedha hizo itakayofanyika jijini Dar es Salaam kesho Machi 29.

Amesema fedha hizo ni pamoja na kuendeleza ujenzi wa shule hiyo ikiwa kwenye muundo wa ghorofa ili iwe na hadhi kama ambavyo inapokea wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Shule hiyo yenye kidato cha kwanza hadi cha sita iliungua moto usiku wa kuamkia Julai 10, mwaka juzi ambapo madarasa tisa ikiwamo maabara na vitu vilivyomo, viti na meza zaidi ya 300 vikiwa na thamani ya Sh bilioni moja.

“Tuliitisha harambee na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kufanikisha kukusanya ahadi na fedha taslimu Sh milioni 4.87 ambapo fedha taslimu zilikuwa Sh milioni 3.64 na tukaanza ujenzi na kampuni ya SUMA JKT kwa usimamizi wa wataalamu wa kutoka Wakala wa Majengo (TBA).

“Awamu ya pili ya Harambee tunatarajia itafanyika jijini Dar es Salaam, Machi 29 yaani kesho katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete,” amesema.

Mkuu wa mkoa ,Zambi aliwataka wananchi, watu wenye makampuni mbalimbali, wadau wa elimu viongozi walioaliwa, waliosoma Lindi nchini kote kujitokeza na kuchangia kwa hali na mali.

Pamoja na mambo mengine, Zambi amesema kwa wanaotaka kuchangia ujenzi huo kwa njia ya simu na kupitia benki, ametoa Akaunti ya Benki ya CRDB Namba 0152208612700 jina la akaunti ni Lindi Education Basket Fund.

“Pia kwa wale ambao watatumia mtandao wa simu Mpesa namba 0768448410 jina Lindi Regional Admistrative na 0685 72 1721 Lindi Sekondari,” amesema.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa mkoa amesema hajisikii vizuri mkoa huo kushika nafasi za mkiani na hivyo aliwataka maofisa wa elimu na wakuu wa shule kuhakikisha wanasimamia shule hiyo inafanya vizuri zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles