28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

BILIONI 1.45 KUNUNUA ARV’S

NA RAMADHAN HASSAN

SERIKALI imeidhinisha jumla ya Sh 1.45 bilioni kwa ajili ya kununulia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVs), Bunge lilielezwa jana.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu, Jenister Mhagama, alitoa kauli hiyo bungeni, ikiwa ni nyongeza ya majibu katika swali lililoulizwa Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii.

Mhagama alisema pesa hizo, mbali na kununua madawa kwa ajili ya kupunguza makali, lakini pia zinalenga kujenga vituo vya kupimia maambukizi katika maeneo ya Mererani na Ziwa Victoria.

Awali Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala, alisema bado wadau wa maendeleo wanaendelea kutoa msaada wa dawa za kurefusha maisha (ARVs), mbali na kwamba inapinga maadili mbalimbali yasiyoendana na mila na desturi za Kitanzania kwa kutoa miongozo mbalimbali.

Dk. Kigwangala alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Magereli (Chadema), ambaye alitaka kujua serikali imejipangaje kuendelea kutoa huduma zilizokuwa zikitolewa na wafadhili, hususan dawa za kurefusha maisha.

Mbunge huyo alisema kwa mujibu wa ripoti ya Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi ya Februari 2017, fedha za wafadhili zinaendelea kupungua na baadhi yake kuwa na masharti yasiyoendana na desturi za Tanzania.

Naibu Waziri alisema serikali inajipanga vema kuhakikisha upatikanaji, hususan wa dawa za kurefusha maisha.

“Serikali kwa sasa imeanzisha mfuko maalumu wa Ukimwi unaojulikana kama Aids Trust Fund (ATF) na mfuko huu utachangiwa na serikali, mashirika/sekta binafsi pamoja na wahisani,” alisema Kigwangala.

Alisema lengo kuu la mfuko (ATF) ni kuchangia upatikanaji wa dawa za kurefusha maisha hapa nchini na akatoa wito kwa watu mbalimbali kuunga mkono juhudi za serikali.

Waziri wa Afya, Ummi Mwalimu, aliwataka wanaume wa Kitanzania kujenga tabia ya kupima na kuchukua dawa za kupunguza makali hayo, kwani kati ya waliopima, wanawake wamekuwa wakichukua dawa, lakini wanaume hawaendi kuchukua.

Mwalimu alisema kati ya waliopima, ni asilimia 48 ya wanaume ndiyo huchukua ARVs, wakati wanawake ni asilimia 70, huku akitaja maambukizi kwa watoto wa kike wa umri wa miaka 15- 24 kwamba yapo kwa asilimia 24, wakati umri kama huo kwa wanaume maambukizi ni asilimia 8.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles