31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Bila baiskeli hakuna harusi Rwanda

JOSEPH HIZA NA MTANDAO

WILAYA ya Bugesera, kusini mashariki mwa Rwanda, ndoa haiwezi kufanyika bila bibi harusi kuambatanisha zawadi ya baiskeli.

Ni hali ambayo ingevutia macho ya hadhila katika maeneo mengine ya nchi.

Katika jamii nyingi za Kiafrika, ni kama mwiko vile mwanamke kuendesha baiskeli, lakini si katika wilaya hii iliyopo katika Jimbo la Mashariki.

Wanaume katika wilaya hii, hawatazami uzuri wa uso, umbo, urembo au tabia linapokuja suala la kuchagua mwanamke wa kumuoa.

Kitu kinachowavutia ni iwapo mwanamke huyo anajua kuendesha baiskeli au la.

Ni kifaa muhimu mno katika maisha ya wanawake wa eneo hilo na inachukuliwa kuwa ‘roho’ ya ndoa zao.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=Fa7Z4Lcybrk[/embedyt]Kwa sababu hiyo, wakati wa kufunga ndoa bibi harusi mtarajiwa yuko tayari kuachana na kile kitu kama mkoba mzuri, viatu au nguo nzuri si baiskeli.

Vitu hivyo kwa kawaida huwa katika furushi la zawadi linaloenda kwa bwana harusi.

Mwanamke asiye na baiskeli nyumbani au asiyejua kuendesha baiskeli anaonekana kuwa hafai kuoa.

Kwa kifupi, mwendo ambao ungefanyika kwa saa moja huwa inakuchukua nusu saa tu kutumia baiskeli.

Haya yote yako katika taifa zima la Rwanda bali katika wilaya hiyo, ambayo iko eneo tambarare, ambako ni rahisi sana kwa matumizi ya baiskeli.

Lakini kubwa zaidi hapa ni kwamba kabla ya ndoa, bibi harusi lazima aweke baiskeli kama zawadi ya kwanza miongoni mwa zawadi nyingi anazompelekea mumewe.

“Mimi niliolewa mwaka 2008, baiskeli niliinunua kwa franga 80,000 kama Sh 220,000 hivi za Tanzania,” anasema Donathe Mukabaruta.

Anasema hayo huku akiendesha baiskeli iliyosheheni madumu matano ya maji, ambayo ni sehemu ndogo tu ya shughuli nyingi za nyumbani anazofanya kila siku kwa kutumia baiskeli

“Baiskeli ndiyo maisha ya kila siku hapa. Inatusaidia katika shughuli za nyumbani, yaani baiskeli ni jibu kwa kila swali katika kazi za nyumbani kama vile kwenda sokoni, kuchota maji au kutafuta lishe ya mifugo.

“Hakuna hata kufikiria kuhusu zawadi nyingine. Kitu cha kwanza unachofikiria ni kununua baiskeli miongoni mwa zawadi nyingi unazompelekea mumeo,” anasema.

Baiskeli ni kitu cha lazima. Huo ndio utamaduni wetu na tunaamini kwamba ukishaipata una uhakika kwamba harusi haiwezi kuvunjika,” anaendelea kufichua.

Ni eneo lenye kasi kubwa ya maendeleo kukiwa na ujenzi wa uwanja wa kisasa wa kimataifa wa ndege na miundombinu mingine ikiwamo barabara.

Wakazi wa eneo hilo wanasema kasi hiyo ya maendeleo ya miundombinu si mwisho wa umaarufu wa baiskeli katika eneo hili kwani masharti ya ujenzi wa barabara lazima yazingatie watumiaji wa baiskeli.

“Kila msichana hapa lazima ajue kuendesha baiskeli,” anasema Donathe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles