23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

‘BIFU’ LA P-SQUARE LAHAMIA KWA WAKE ZAO

LAGOS, NIGERIA


MWEZI mmoja uliopita kulikuwa na taarifa ya kuvunjika kwa kundi la P-Square, ambalo lilikuwa linaundwa na mapacha Peter na Paul pamoja na kaka yao Jude Okoye, lakini taarifa mpya ni kwamba wake wa wasanii hao na wao wameingia kwenye bifu lao.

Jumatano iliopita Jude aliposti picha ya mtoto wake kwenye ukurasa wake wa Instagram, hivyo Paul na mke wake Anita wakaamua kuichukua picha hiyo na kuiposti kwenye akaunti yao.

Utata umekuja mara baada Paul ‘kuitag’ picha hiyo kwa Jude na mke wake Ifeoma, lakini Anita aliamua ‘kuitag’ kwa Jude peke yake badala na mke wake.

Taarifa za chini chini zinasema kwamba, Anita aliamua kufanya hivyo kwa kuwa Ifeoma hataki kumfuata mwenzake huyo kwenye akaunti ya Instagram, hivyo wawili hao hawana maelewano.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles